Content removal request!


FULL HIGHLIGHTS: YANGA SC 3-1 STAND UNITED - VPL 12/03/2018

Hatimaye Yanga imefanikiwa kuwashika mahasimu wake Simba SC kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kwa kufikisha pointi 46, huku ikiendelea kubaki nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao, licha ya Simba kuwa na kiporo cha mchezo mmoja mkononi. Yanga imefanikiwa kufikia hatua hiyo baada ya kuichapa Stand United kutoka Shinyanga jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa raundi ya 22 wa ligi hiyo uliopigwa leo kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam. Magoli ya Yanga yamefungwa na Ally Ally likiwa ni la kujifunga dakika ya 7, Ibrahim Ajib dakika ya 12 na Obrey Chirwa dakika ya 85 wakati bao pekee la Stand likifungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 82. Hata hivyo Stand United watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi za wazi zaidi ya tano kwa washambuliaji wake kutokuwa makini kila wanapofika langoni kwa Yanga. Tazama kwa ufupi jinsi mambo yalivyokuwa.