Bao pekee kutoka kwa beki Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ limetosha kuipa Yanga pointi tatu mbele ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Ninja amefunga goli hilo kwa kichwa dakika ya 64 akimalizia mpira wa adhabu ndogo ulipigwa na Ibrahim Ajibu, bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo na kuendeleza rekodi ya ushindi na kutopoteza mchezo kwa Yanga tangu kuanza kwa ligi msimu huu. Ushindi huo unaifanya Yanga izidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 47, mbele ya Azam wenye pointi 40 na Simba wenye pointi 30.
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imefanya kweli baada ya kuinyuka mabao 2-1 Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliomalizika kwenye Uwanja wa Azam Complex leo Alhamisi usiku. Ushindi huo unaihakikishia Azam FC nafasi ya kuendelea kubakia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 33 baada ya kushinda mechi 10 na sare tatu ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.
Azam FC imepata ushindi wa mabao 2-1 ikiwa kwenye Dimba lake la nyumbani Azam Complex Chamazi Dar es Salaam dhidi ya Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi. Mabao ya Azam kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ dakika ya 11 ya mchezo na Tafadzwa Kutinyu dakika ya 66 huku bao pekee la Ruvu Shooting likifungwa na Said Dilunga dakika ya 27. Matokeo haya yanaifanya Azam FC kufikisha pointi 33 kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imecheza jumla ya mechi 13 huku ikiendelea kulinda rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote hadi sasa tangu kuanza kwa ligi msimu huu.
#SIMB SC VS #JKTTanzania Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Kikosi cha klabu ya Simba kimewasil salama Tanga kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania. Kuelekea mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi ya wikiendi ijayo, uongozi umesema hali na morali ya wachezaji ipo vizuri. Mabingwa hao watetezi wa ligi wanaenda kucheza na JKT wakiwa na alama 23 katika nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi. Wakati huo JKT ambao watakuwa nyumbani watapepetuana na Simba wakiwa na alama 18 kwenye msimamo wa ligi. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars OKWI, CHAMA, KWASI NA SALAMBA WOTE WAFUNGA SIMBA SC YAIKANDAMIZA ALLIANCE FC 5-1 TAIFA MABINGWA watetezi, #SimbaSC wamepata ushindi wa kishindo baada ya kuichapa 5-1 #AllianceFC katika mchezo wa #LigiKuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikiziwa pointi nne na vinara, Azam FC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi. Watani wao wa jadi, Yanga SC wanafuatia kwa pointi zao 19 na kesho watacheza mechi yao ya nane kwa kumenyana na KMC Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa. Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi alifunga bao la kwanza dakika ya 10 kwa kichwa akimalizia pasi ya kocha baada ya krosi ya beki Mghana, Nicholas Gyan baada ya kona fupi kutoka upande wa kulia. Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan/Shomari Kapombe dk46, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Pascal Wawa, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Hassan Dilunga dk61, Clatous Chama, Adam Salamba/Meddie Kagere dk75, John Bocco na Emmanuel Okwi. Alliance FC; Kelvin Richard, Israle Patrick, Hance Masoud, Wema Sadock, Geoffrey Luseke, Juma Nyangi, Dickson Ambundo, Balama Mapinduzi/Martin Kiggi dk89, Michael Chinedu/Juhudi Philemon dk61, Jamal Mtegeta/Zabona Khamis dk80 na Siraj Juma. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
#YANGAvsMBAO MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0 Yanga imefanikiwa kuapata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Taifa Dar es salaam. Bao la kwanza limepachikwa kimiani na Rafel Daud mnamo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kwa njia ya kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajibu. Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, kipindi cha pili Mbao walijitahada kuja kwa kasi kushambulia lango la Yanga lakini haikuweza kusaidia kitu. Licha ya mashambulizi hayo, Mbao FC walipata nafasi zingine kama nne kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia vema. Zikiwa zimeongezwa dakika tano, Ibrahim Ajibu alifanikiwa kuingia kambani kwa kufunga bonge la bao kwa tikitaka ya aina yake na kuifanya Yanga iwe mbele kwa mabao 2-0. Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 2 na Mbao FC 0. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 16 katika msimamo wa ligi huku Mbao ikisalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya 5. GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOKInstall
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA SC imeamsha makali yake baada ya kuichapa African Lyon ya Dar es Salaam mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam usiku wa leo. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, ikijivuta hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Azam FC pointi 15 za mechi saba, Singida United pointi 16 mechi tisa na Mtibwa Sugar pointi 17 mechi tisa. Ushindi wa leo wa Simba SC umetokana na mabao ya kiungo mzalendo, Shiza Ramachani Kichuya kipindi cha kwanza na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi kipindi cha pili, wakati bao la Lyon limefungwa na Awadh Juma dakika ya 62. Kichuya ambaye ameporomoka kiasi cha kuachwa timu ya taifa, leo aliamsha makali yake kwa kufunga bao la kwanza mapema tu dakika ya nane akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga SC umemalizika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Kwa sare hiyo, Yanga SC inajisogeza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutokana na kujiongezea pointi moja na kufikisha 13 baada ya kucheza mechi tano, nne nyingine zote wakishinda. Kwa upande wao, mabingwa watetezi, Simba SC wanafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi sita, wakitoa sare ya pili leo na kufungwa moja, nyingine tatu wakishinda. Lakini Simba SC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na pointi zote kwenye mchezo wa leo, kwani walifanikiwa kuwazidi wapinzani wao muda wote Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars