Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya leo kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Walioitafuna miwa ya Mtibwa kwenye mchezo huo uliokuwa mzuri na wa kuvutia, ni John Bocco dakika ya 33, Clatous Chama dakika ya 48 na Emmanuel Okwi dakika ya 56. Ushindi huo umefanya Simba ifikishe pointi 85 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwaacha Yanga kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 83 wakati Mtibwa Sugar wakisalia kwenye nafasi ya tano na pointi 49.
SIMBA VS MTIBWA SUGAR: Vikosi Vilivyoanza Uwanja wa Uhuru Leo Ni mtanange wa ligi kuu wa kukata na shoka kati ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar, unachezwa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar..... #SIMBAVsMTIBWA https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
SIMBA SC vs MTIBWA SUGAR LEO. Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo katika dimba la Uhuru. Simba SC wametoka kubanwa mbavu mechi iliyopita je leo watarekebisha makosa na kuondoka na ushindi ama watapokea surprise kutoka kwa Mtibwa Sugar? #MagoliYoteSimbanaKageraSugar #simbasctanzania #Azamsports2 #Azamtvapp #mtibwaofficial #SimbaNaMtibwaSugar
__ Harakati za Bongo is an online magazine that specializes in educations stories and entertainment stories from Tanzania. Harakati za Bongo, Aloso abbreviated as HZB was started 2011 by John Sambila,who had a passion for wrinting and photography from the time he was young. ******************************************* Share, Support, Subscribe!!! Subscribe: UC-4fDfmsXy9hIcEmPKbARIQ Youtube: https://www.youtube.com/c/HZBTV Twitter: http://www.twitter.com/harakatizabongo Facebook: http://www.facebook.com/harakatizabongo Instagram: http://instagram.com/harakatizabongo Google Plus: https://plus.google.com/+harakatizabongo Website: http://harakatibongo.com/
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wameng’ang’aniwa kwenye Uwanja wa Uhuru kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC. Timu zote zilionesha soka la kiwango cha juu ambapo Simba walifanya mashambulizi mengi zaidi langoni kwa Azam lakini walishindwa kupata bao kutokana na uimara wa safu ya ulinzi ya Azam iliyokuwa chini ya Agrey Moris na Yakubu Mohamed. Licha ya kushambuliwa zaidi, Azam walipoteza nafasi mbili za wazi kupitia kwa Donald Ngoma dakika ya 29 na Obrey Chirwa dakika ya 87, hivyo mchezo kumalizika kwa suluhu. Matokeo hayo yanaifanya Simba kubakiza pointi nane pekee ili kutetea taji lake, ikiwa imefikisha pointi 82 na mechi tano mkononi, wakati wapinzani wao wa karibu, Yanga wakiwa na pointi 81 na mechi tatu mkononi. Azam wao wanaendelea kukaa nafasi ya tatu wakifikisha pointi 69 na mechi mbili mkononi.
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Kocha wa Azam FC, Meja Abdul #Mingange amesema, kikosi chao cha #AzamFC hakijafikia malengo waliyokusudia labda wachukue ubingwa wa FA utakaowapa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na akaweka wazi kuwa suluhu yao na Simba imewapata walichotaka. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Amesema, malengo ya Azam FC yalikuwa ni kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara au wamalize nafasi ya pili kwa sababu timu yao ni kubwa. "Katika msimu huu sisi hatujafanya vizuri kwa sababu tulitakiwa kuchukua ubingwa au nafasi ya pili lakini kama tutachukua ubingwa wa FA angalau tutakuwa tumefanya kitu,"alisema Mingange aliyechukua mikoba ya kuinoa Azam FC baada ya kutimuliwa Kocha Mholanzi Hans Pluijm. Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars "Wenzetu Simba walikuwa wanatafuta ubingwa lakini sisi hatuko huko hivyo hatukutaka kujichosha ndiyo maana tulicheza kwa kuzuia ili tusifungwe hivyo tumepata tulichokitaka,"alisema Mingange. Hata hivyo, Mingange amesema mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha Uwanja wa Uhuru ambao walichezea mechi kujaa maji uliwaathiri wao na wapinzani wao. Twitter: https://twitter.com/kidanistars Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei/John Bocco dk79, Haruna Niyonzima, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Clatous Chama. Azam FC; Razack Abalora, Nickolas Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Joseph Mahundi, Frank Domayo, Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Ramadhan Singano/Daniel Lyanga dk53.
Timu ya African Lyon ya Jijini Dar es Salaam, imeshuka rasmi daraja na sasa itakwenda kucheza Ligi Daraja la Kwanza baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mbao FC kwenye dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa 34 wa Ligi Kuu kwa African Lyon, magoli ya wageni Mbao FC yamefungwa na Evageristus Mujwahuki dakika ya 3, Pastory Athanas dakika ya 27 na Said Hamis Said Jr dakika ya 40 kwa mkwaju wa penati. Magoli ya wenyeji African Lyon yamefungwa na Adili dakika ya 8 kwa penati na Said Mtikila dakika ya 72. Lyon imebaki mkiani ikiwa na alama 22, hivyo kushuka daraja rasmi kwani hata ikishinda mechi zake zote nne zilizosalia, haiwezi kuifikia Mwadui FC ambayo ndiyo iliyo juu yake ikiwa na pointi 37.
KIKOSI cha Maangamizi cha SIMBA VS KAGERA SUGAR Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa Simba kuendelea kuwa kibonde wa Kagera Sugar baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0. Bao pekee la mchezo huo limepatikana mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza kwa Mohammed Hussein kujifunga ikiwa ni baada ya kukosa mawasiliano mazuri baina yake na kipa Aishi Manula kufuatia mpira uliopigwa na mchezaji wa Kagera. Licha ya kutawala sehemu kubwa ya mchezo, Kagera Sugar walionekana kulinda kwa umakini zaidi lango haswa baada ya kupata bao la kuongoza na kuwafanya Simba kushindwa kucheka na nyavu zao. Kunako kipindi cha pili cha mchezo, Kocha wa Simba Patrick Aussems aliwafanyia mabadiliko wachezaji Hassan Dilunga aliyemtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Rashid Juma huku James Kotei naye akitolewa na Jonas Mkude akichukua nafasi yake. Mabadiliko hayaikuisaidia chochote Simba ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalisalia kuwa 1-0. Kuendelea kupoteza kwa Simba dhidi ya Kagera kunawafanya wazidi kusalia nafasi ya kwanza wakiwa na alama zao 81 kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi huku Kagera wakijiongezea alama tatu muhimu wakifikisha alama 43. #SIMBASC https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho