Content removal request!


AFRICAN LYON 2-3 MBAO FC; FULL HIGHLIGHTS (TPL - 09/05/2019)

Timu ya African Lyon ya Jijini Dar es Salaam, imeshuka rasmi daraja na sasa itakwenda kucheza Ligi Daraja la Kwanza baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mbao FC kwenye dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa 34 wa Ligi Kuu kwa African Lyon, magoli ya wageni Mbao FC yamefungwa na Evageristus Mujwahuki dakika ya 3, Pastory Athanas dakika ya 27 na Said Hamis Said Jr dakika ya 40 kwa mkwaju wa penati. Magoli ya wenyeji African Lyon yamefungwa na Adili dakika ya 8 kwa penati na Said Mtikila dakika ya 72. Lyon imebaki mkiani ikiwa na alama 22, hivyo kushuka daraja rasmi kwani hata ikishinda mechi zake zote nne zilizosalia, haiwezi kuifikia Mwadui FC ambayo ndiyo iliyo juu yake ikiwa na pointi 37.