Alichosema Kocha wa Azam baada ya kuigomea Simba
Alichosema Kocha wa Azam baada ya kuigomea Simba

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Kocha wa Azam FC, Meja Abdul #Mingange amesema, kikosi chao cha #AzamFC hakijafikia malengo waliyokusudia labda wachukue ubingwa wa FA utakaowapa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na akaweka wazi kuwa suluhu yao na Simba imewapata walichotaka. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Amesema, malengo ya Azam FC yalikuwa ni kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara au wamalize nafasi ya pili kwa sababu timu yao ni kubwa. "Katika msimu huu sisi hatujafanya vizuri kwa sababu tulitakiwa kuchukua ubingwa au nafasi ya pili lakini kama tutachukua ubingwa wa FA angalau tutakuwa tumefanya kitu,"alisema Mingange aliyechukua mikoba ya kuinoa Azam FC baada ya kutimuliwa Kocha Mholanzi Hans Pluijm. Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars "Wenzetu Simba walikuwa wanatafuta ubingwa lakini sisi hatuko huko hivyo hatukutaka kujichosha ndiyo maana tulicheza kwa kuzuia ili tusifungwe hivyo tumepata tulichokitaka,"alisema Mingange. Hata hivyo, Mingange amesema mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha Uwanja wa Uhuru ambao walichezea mechi kujaa maji uliwaathiri wao na wapinzani wao. Twitter: https://twitter.com/kidanistars Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei/John Bocco dk79, Haruna Niyonzima, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Clatous Chama. Azam FC; Razack Abalora, Nickolas Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Joseph Mahundi, Frank Domayo, Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Ramadhan Singano/Daniel Lyanga dk53.





Popular Tags

#Neymar  #Kawhi Leonard  #Paul Pogba  #Kyrie Irving  #Kobe Bryant  #Mesut Ozil  #Los Angeles Lakers  #Philadelphia 76ers  #Paul George  #Best Goalkeeper Saves  

Popular Users

#itsBayleyWWE  #TheNotoriousMMA  #CP3  #JoelEmbiid  #Cristiano  #ddlovato  #ArianFoster  #DwyaneWade  #rihanna  #imVkohli  #Joey7Barton  #MieshaTate  #SHAQ  #dougferguson405  #NiallOfficial