Shabiki wa Yanga Atoa Povu Kisa Kipigo cha Mtibwa
Shabiki wa Yanga Atoa Povu Kisa Kipigo cha Mtibwa

Baada ya Yanga kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar,nahodha wa timu hiyiop Ibrahim Ajib amewatupia lawama waamuzi kuwa wamekuwa hawaitendei haki timu yao katika mechi nyingi za Ligi Kuu Bara. Bao la Riphat Khamis dakika ya 52 lilitosha kuipa ushindi Mtibwa Sugar na kuendeleza rekodi yao bora inapocheza nyumbani kwani katika michezo mitano mfululizo iliyopita iliyocheza Morogoro imeshinda yote. Kukataliwa kwa bao lililofungwa na Amissi Tambwe dakika ya 89 ndiko kulisababisha Ajib kutoa ya moyoni ukuhusu waamuzi kuwa wamekuwa hawatendi haki licha ya wachezaji kupambana sana uwanjani kutafuta matokeo. Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga alikataa bao hilo baada ya kumuangalia mwamuzi wa pembeni ambaye alinyoosha kibendera kuashiriki mfungaji alikuwa ameotea. "Waamuzi hawachezeshi kwa haki kwani huwa hawako upande wetu mechi nyingi. Kwani tunajitahidi kwa uwezo wetu lakini inaumiza unapambana sana lakini anatokea mwingine anakurudisha nyuma"alisema. Ajib amesema wataendela kupambana katika michezo iliyobaki kwani licha ya wapinzani wao Simba ambao wanawafuukuza wana mechi nyingi hivyo lolote. Kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Meddie Kagere amefunga mabao mawili na kuikoa timu yake isipate kipigo kutoka kwa Coastal Union. Simba ilijikuta ikishangazwa dakika ya kwanza tu baada ya Raizin Hafidhi kuifungia Coastal Union bao kutokana na beki Erasto Nyoni kujichanganya na kipa wake Aishi Manula katika kuokoa mpira huo. Kagere aliisawazishia Simba bao kwa penalti dakika ya 48, penalti iliyotokana na Emmanuel Okwi kuangushwa na kipa wa Coastal Union Sudi Mohammed. Dakika ya 68 Kagere aliipata Simba bao la pili kwa shuti kali akimalizia pasi ya Clatous Chama hivyo kufikisha mabao 16 kwenye ligi na kumfikia kinara Salum Aiyee wa Mwadui FC huku akimzidi bao moja Heritier Makambo wa Yanga mwenye mabao 15.



Sababu mbili mechi ya Simba vs JKT kuahirishwa na hatma ya mashabiki waliokata tiketi
Sababu mbili mechi ya Simba vs JKT kuahirishwa na hatma ya mashabiki waliokata tiketi

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania uliokuwa uchezwe leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umeahirishwa kutokana na hali ya mvua ambayo imesababisha uwanja kujaa maji. Mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine. Katibu wa Chama cha Soka mkoa wa Morogoro Charles Mwakambaya anaeleza ni kwanini mechi hiyo haikupangwa kuchezwa kesho kama inavyoelekezwa na kanuni huku akieleza pia hatma ya mashabiki ambao tayari walishakata tiketi



Mvua Kubwa ilivyozuia Mechi ya SIMBA SC na JKT Tanzania leo
Mvua Kubwa ilivyozuia Mechi ya SIMBA SC na JKT Tanzania leo

Mvua Kubwa iliyozuia Mechi ya SIMBA SC na JKT Tanzania leo. Uwanja wa Jamuhuri Mjini Morogoro wajaa MAJI kutokana na Mvua kubwa iliyonyesha na kufanya Mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania siku ya leo kuhairishwa. Morogoro



Simba sc Walivyoingia Kuikabili JKT Tanzania Uwanja Umejaa Maji Morogoro
Simba sc Walivyoingia Kuikabili JKT Tanzania Uwanja Umejaa Maji Morogoro

SUBSCRIBE HAPA https://www.youtube.com/channel/UC_m6Lmu4NexLFzafJH5InYA/videos?view_as=subscriber tembelea WEBSITE YETU https://bmtvtanzania.com/ INSTAGRAM https://www.instagram.com/bmtvtanzania FACEBOOK https://www.facebook.com/bmtvtanzania TWITTER https://twitter.com/bmtvtanzania1



Uchambuzi Wa Mwalimu Kashasha full Time Simba 3 Mbao 0 , Bocco, Kagere Wacheka na nyavu
Uchambuzi Wa Mwalimu Kashasha full Time Simba 3 Mbao 0 , Bocco, Kagere Wacheka na nyavu

DAKIKA 90 za mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao zimekamilika uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. John Bocco alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Bocco alipachika bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Mbao FC, Peter Mwangosi kunawa mpira uliopigwa na Mzamiru Yassin dakika ya 58. Meddie Kagere alipachika bao la tatu kwa Simba baada ya beki  wa Mbao kumchezea rafu Kagere eneo la hatari na mwamuzi kutoa penalti iliyopigwa na Kagere dakika ya 79.



Kocha Mbao: Tufungwa na Simba 3-0, Tumefanya Makosa
Kocha Mbao: Tufungwa na Simba 3-0, Tumefanya Makosa

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars #SIMBASC imeendeleza furaha kwa mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya #MbaoFC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya Nahodha John Raphael Bocco na Mnyarwanda Meddie Kagere unaifanya Simba SC ifikishe pointi 57 baada ya kucheza mechi 22, lakini inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 59 na Yanga SC pointi 67 baada ya wote kucheza mechi 28. Bocco, mmoja wa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichokata tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa uya Afrika mwaka huu nchini Misri wiki iliyopita, alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 25 akimalizia krosi ya beki wa kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars



FT: SIMBA 3-0 MBAO FC, Mashabiki Wajitokeza Jamhuri Moro
FT: SIMBA 3-0 MBAO FC, Mashabiki Wajitokeza Jamhuri Moro

#SimbaSC Vs MbaoFC Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars DAKIKA 90 za mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao zimekamilika uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. John Bocco alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Bocco alipachika bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Mbao FC, Peter Mwangosi kunawa mpira uliopigwa na Mzamiru Yassin dakika ya 58. Meddie Kagere alipachika bao la tatu kwa Simba baada ya beki wa Mbao kumchezea rafu Kagere eneo la hatari na mwamuzi kutoa penalti iliyopigwa na Kagere dakika ya 79. Simba leo wameanzisha jeshi lao kamili huku mlinda mlango namba moja Aishi Manula akiwa ameanzia benchi akimtazama Deogratius Munish. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars




« Previous Next »


Popular Tags

#Best Goals  #James Harden  #Best Champions League  #Stephen Curry  #Thomas Muller  #Los Angeles Lakers  #Stephen Curry  #Goalkeeper Saves  #Counter Attack Goals Football  #Mesut Ozil  

Popular Users

#GNev2  #nfl  #incarceratedbob  #THNRyanKennedy  #KevinHart4real  #UKCoachCalipari  #sportspickle  #ArianaGrande  #Buccigross  #Joey7Barton  #RSherman_25  #ddlovato  #TheChristinaKim  #darrenrovell