Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania uliokuwa uchezwe leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umeahirishwa kutokana na hali ya mvua ambayo imesababisha uwanja kujaa maji. Mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine. Katibu wa Chama cha Soka mkoa wa Morogoro Charles Mwakambaya anaeleza ni kwanini mechi hiyo haikupangwa kuchezwa kesho kama inavyoelekezwa na kanuni huku akieleza pia hatma ya mashabiki ambao tayari walishakata tiketi