Content removal request!


Uchambuzi Wa Mwalimu Kashasha full Time Simba 3 Mbao 0 , Bocco, Kagere Wacheka na nyavu

DAKIKA 90 za mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao zimekamilika uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. John Bocco alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Bocco alipachika bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Mbao FC, Peter Mwangosi kunawa mpira uliopigwa na Mzamiru Yassin dakika ya 58. Meddie Kagere alipachika bao la tatu kwa Simba baada ya beki  wa Mbao kumchezea rafu Kagere eneo la hatari na mwamuzi kutoa penalti iliyopigwa na Kagere dakika ya 79.