Content removal request!


COASTAL UNION 1-1 MBAO FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 28/09/2018)

Coastal Union ya Jijini Tanga imepata sare ya bao 1-1 na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini humo. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Ayoub Lyanga dakika ya 31 kabla ya Mbao kureje kwa nguvu zaidi kipindi cha pili na kusawazisha kupitia kwa said Hamis Said Jr dakika ya 50. Baada ya mchezo huo makocha wa timu zote mbili Amri Said wa Mbao na Juma Mgunda wa Coastal Union wameuzungumzia mchezo huo