Mbao FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Bao hilo pekee limepatikana katika dakika ya nne kati ya dakika tano za nyongeza kupitia kwa mshambuliaji wake Ndaki Robert.