Content removal request!


“…unaweza ukaumia” - Alikiba ataja kinachomfanya asionekane dimbani kwenye mechi za TPL?

Mchezaji wa Coastal Union ambaye pia ni msanii wa bongo fleva, Alikiba ametegua kitendawili kuhusu siku ambayo ataanza rasmi kucheza kwenye mfululizo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Kiba amezungumza na Azam TV mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani Jijini Tanga na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Katika mahijiano haya pia Alikiba ameichambua timu yake kwa jinsi alivyoutazama mchezo. Mchezaji huyo aliyesajiliwa Coastal Union msimu huu, hajacheza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa mwezi Agosti.