Timu ya Mbao FC imefufua matumaini ya kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda SC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Bao pekee la ushindi la Mbao FC limefungwa na Said Hamis Said Jr dakika ya 57 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea mpira uliopigwa kutoka kwa kipa wake Bruno Thomas na kuwatoka mabeki wa Ndanda. Ushindi huo umeitoa Mbao kutoka nafasi ya 19 hadi ya 13 ikifikisha pointi 40 huku Ndanda ikisalia na pointi 43 nafasi ya saba.
Goli pekee la EMMANUEL OKWI halikuweza kuendeleza ushindi. FT: KAGERA SUGAR 2-1 SIMBA Baada ya kipigo cha goli 2-1 toka kwa Kagera sugar siku ya leo, Simba inakuwa imepoteza mechi 2 kati ya 24 ilizocheza kwenye ligi msimu huu. Michezo hiyo ni dhidi ya Mbao FC ambapo Simba ilifungwa 1-0 pamoja na mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar 2-1.
DAKIKA 90 za mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao zimekamilika uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. John Bocco alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Bocco alipachika bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Mbao FC, Peter Mwangosi kunawa mpira uliopigwa na Mzamiru Yassin dakika ya 58. Meddie Kagere alipachika bao la tatu kwa Simba baada ya beki wa Mbao kumchezea rafu Kagere eneo la hatari na mwamuzi kutoa penalti iliyopigwa na Kagere dakika ya 79.
Huu ni mchezo wa 10 wa simba inashinda mfululizo kwenye ligi kuu tanzania bara akifikisha alama 57, alama 10 nyuma ya yanga yenye alama 67, simba ina faida ya michezo sita mkononi.
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars #SIMBASC imeendeleza furaha kwa mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya #MbaoFC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya Nahodha John Raphael Bocco na Mnyarwanda Meddie Kagere unaifanya Simba SC ifikishe pointi 57 baada ya kucheza mechi 22, lakini inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 59 na Yanga SC pointi 67 baada ya wote kucheza mechi 28. Bocco, mmoja wa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichokata tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa uya Afrika mwaka huu nchini Misri wiki iliyopita, alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 25 akimalizia krosi ya beki wa kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars