Timu ya Mbao FC imefufua matumaini ya kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda SC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Bao pekee la ushindi la Mbao FC limefungwa na Said Hamis Said Jr dakika ya 57 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea mpira uliopigwa kutoka kwa kipa wake Bruno Thomas na kuwatoka mabeki wa Ndanda. Ushindi huo umeitoa Mbao kutoka nafasi ya 19 hadi ya 13 ikifikisha pointi 40 huku Ndanda ikisalia na pointi 43 nafasi ya saba.