Simba SC imetinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports #AzamSportsFederationCup baada ya kuichapa Pamba FC kutoka Jijini Mwanza, mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Magoli ya Simba kwenye mchezo huu yamefungwa na Peter Banda, Kibu Denis na Yusuph Mhilu aliyefunga magoli mawili.
Ruvu Shooting wametoka nyuma na kupata pointi tatu muhimu dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Dimba la Mabatini mkoani Pwani. Geita wametangulia kupata bao kupitia kwa Offen Chikola kipindi cha kwanza kabla ya Ruvu Shooting kurejea kipindi cha pili na nguvu mpya wakipa mabao mawili kupitia kwa Hamadi Majimengi pamoja na Elias Maguli. Haya hapa magoli yote matatu
Azam FC imepoteza mchezo wake wa tisa kwenye ligi kuu msimu huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mbeya City... Mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Magoli ya Mbeya City kwenye mchezo huu yamefungwa na Juma Shemvuni pamoja na beki wa Azam FC, Daniel Amoah aliyejifunga dakika ya 83 huku goli pekee la Azam likifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 88.

Kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu, Yanga imepata ushindi dhidi ya Namungo FC ikiitandika mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Yanga ndiyo waliotangulia kwa goli la Fiston Mayele kabla ya Shiza Kichuya kuchomoa dakika ya 33, lakini Feisal Salum akaiongezea Yanga bao dakika ya 39 na mechi kumalizika kwa ushindi wa kwanza tangu Namungo ipande daraja msimu wa 2019/20.

Simba SC imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa kwenye Dimba la Mkwakwani jijini Tanga. Simba wametangulia kwa bao la Bernard Morrison dakika ya 40, kabla ya Coastal kusawazisha kwa goli la Victor Akpan dakika ya 78 lakini Medie Kagere akaweka la pili dakika za nyongeza. Haya hapa magoli yote
SHABIKI wa COASTAL UNION Aliyeingia na PEMPERS Uwanjani AWAVALISHE SIMBA AUMBUKA - "NIMEBAKI NAYO" DAKIKA 90 za mtanange wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Coastal Union vs Simba SC, zimemalizika kwa mnyama kuvuna alama 3 kwa kuwatandika Coastal mabao mawili kwa moja. ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: https://www.youtube.com/playlist?list=PL22mc2rU91vDNQjLA5ikELAOcJp5XrakD ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 712 101 629), ( +255 784 888982) ⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: https://www.youtube.com/playlist?list=PL22mc2rU91vD-h-a328gR3qltQXYWVQiO ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua ⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews ⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline