Ruvu Shooting wametoka nyuma na kupata pointi tatu muhimu dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Dimba la Mabatini mkoani Pwani. Geita wametangulia kupata bao kupitia kwa Offen Chikola kipindi cha kwanza kabla ya Ruvu Shooting kurejea kipindi cha pili na nguvu mpya wakipa mabao mawili kupitia kwa Hamadi Majimengi pamoja na Elias Maguli. Haya hapa magoli yote matatu