Simba SC imetinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports #AzamSportsFederationCup baada ya kuichapa Pamba FC kutoka Jijini Mwanza, mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Magoli ya Simba kwenye mchezo huu yamefungwa na Peter Banda, Kibu Denis na Yusuph Mhilu aliyefunga magoli mawili.