Azam FC imelazimishwa suluhu na Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa usiku wa Septemba 28, 2018 kwenye dimba la Azam Complex Chamazi. Katika mchezo huo Lipuli FC walionakana kucheza kwa mbinu ya kujilinda zaidi huku wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa Azam FC lakini hadi mwisho wa mchezo hapakuwa na bao lolote. Kwa mara ya kwanza leo Donald Ngoma ameanza kuitumikia Azam FC kwenye mechi za Ligi Kuu na amekumbana na matukio haya mawili ambapo moja limezua utata kuwa huenda ilipaswa kuwa penati. Tazama Highlights, kisha toa maoni yako, Je, matukio hayo yalipaswa kuwa penati?
Ilikuwa ni free-kick iliyopigwa na Biashara United, na mpira uzama kimiani, lakini mwamuzi wa pembeni akaamua kuwa ilikuwa ni off side. Ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani Jijini Tanga, Agosti 25, mwaka huu. Itazame, kisha toa maoni yako, wewe umeionaje?
Timu ya Coastal Union ya Tanga imepata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la CCM Mkwakwani, Jijini Tanga. Bao pekee la Coastal Union kwenye mchezo huo limefungwa na Haji Ugando dakika ya 20 ya mchezo. Katika mchezo huo, Coastal walianza kwa kasi na kufanikiwa kutikisa nyavu dakika ya 4 lakini ilikuwa ni off side, na kisha kupata penati dakika ya 13 lakini Mkwaju wa Mtenje Juma ukapanguliwa na kipa wa Biashara United Balora Nasridine. Biashara United walionekana kumlalamikia mwamuzi wa pembani baada ya kukataa bao lao la dakika ya 45 kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea. Mara baada ya mchezo, manahodha wa pande zote mbili wamezungumza. Tazama highlights.
Mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil alifanya jambo ambalo lilisisimua uwanja mzima baada ya kutupiwa kipande cha mkate na shabiki. Ozil alichofanya ni kuchukua mkate ule na kuubusu kisha kuuweka pembeni ili kuonyesha kuwa anaheshimu chakula.
Timu ya Singida United imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo kwenye dimb la Namfua, mjini Singida. Mchezo huo umelazika kuchezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1. JKT ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 38 kupitia kwa Hassan Matelema na kisha Singida kusawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Tafadzwa Kutinyu, ambaye pia ndiye aliyefunga bao la pili katika dakika ya 98. Haya ndiyo mabao yenyewe.
Msemaji wa Simba Haji Manara Ameropoka tena leo baada ya kuizamisha Azam bao 1 kwa 0 jana CLICK SUBSCRIBE KISHA LIKE NA COMMENT ILI UWEZE KUPATA HABARI NYINGINE KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI.
Ni mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) uliopigwa leo katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Mbao ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 3, kisha Mbeya City wakakosa mkwaju wa penati dakika ya 5 kupitia kwa Mohamed Samatta.