Timu ya Singida United imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo kwenye dimb la Namfua, mjini Singida. Mchezo huo umelazika kuchezwa kwa dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1. JKT ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 38 kupitia kwa Hassan Matelema na kisha Singida kusawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Tafadzwa Kutinyu, ambaye pia ndiye aliyefunga bao la pili katika dakika ya 98. Haya ndiyo mabao yenyewe.