Azam FC imelazimishwa suluhu na Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa usiku wa Septemba 28, 2018 kwenye dimba la Azam Complex Chamazi. Katika mchezo huo Lipuli FC walionakana kucheza kwa mbinu ya kujilinda zaidi huku wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa Azam FC lakini hadi mwisho wa mchezo hapakuwa na bao lolote. Kwa mara ya kwanza leo Donald Ngoma ameanza kuitumikia Azam FC kwenye mechi za Ligi Kuu na amekumbana na matukio haya mawili ambapo moja limezua utata kuwa huenda ilipaswa kuwa penati. Tazama Highlights, kisha toa maoni yako, Je, matukio hayo yalipaswa kuwa penati?