Yanga SC imelipa kisasi kwa kuitandika Azam FC mabao 2-1 kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.... Yanga imepata mabao yake yote mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Pacome Zouzoua dakika 11 na Prince Dube dakika ya 34, huku Azam FC wakipata bao lao dakika ya 81. Tazama magoli....
Super Sub, Elvis Rupia amefunga goli pekee na la ushindi wa bao 1-0 kwa Singida Black Stars dhidi ya Azam FC, mchezo wa Ligi kuu ya NBC ukipigwa kwenye Uwanja wa Liti, Singida. Goli kwa Azam FC ni Zuberi Foba ambaye hata hivyo kabla ya goli hili la dakika ya 75, alikuwa amefanya saves kadhaa na kuzuia hatari nyingi za Singida Black Stars....
Magoli kutoka kwa Israel Patrick Mwenda, Clement Mzize na Prince Dube yameipa Yanga ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC ukipigwa kwenye Dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Hiki ni kisasi kwa Yanga dhidi ya Tabora United, ikikumbkwa mchezo wa kwanza waliokutana msimu huu, Yanga ilipoteza nyumbani kw akichapo cha mabao 3-1 kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.
Ni mechi ya kirafiki iliyoshindwa kumalizika baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha mjini Singida na mechi kuahirishwa ikiwa imechezwa kwa dakika 57 pekee. Hadi muda huo, ubao ulikuwa ukisomeka 1-1, wakianza Yanga dakika ya kupitia kwa Jonathan Ikangalombo na kisha Singida kusawazisha dakika ya 56 kupitia kwa Marouf Tchakei. Ni Singida Black Stars dhidi ay Yanga, mchezo maalum wa kuzindua Uwanja mpya wa Airtel unaomilikiwa na klabu ya Singida Black Stars. Haya hapa magoli…
Simba SC imeipa kichapo cha mabao 6-0 Dodoma Jiji FC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la KMC, Dar es Salaam. Elie Mpanzu ndiye aliyeitanguliza Simba dakika ya 16 na kisha Jean Charles na Kibu Denis wakafunga mawili kila mmoja huku linguine likiwekwa nyavuni na Steven Desse Mukwala…
Yanga SC imeichapa Coastal Union mabao 3-1 na kutinga 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank, mchezo ukipigwa kwenye Dimba la KMC Complex. Maxi Nzengeli amefunga magoli mawili dakika ya 2 na 15, wakati Clement Mzize akipiga la tatu dakika ya 21 baada ya Coastal Union kupata bao la dakik aya 18 kupitia kwa Miraji Abdallah. Magoli yote yamefungwa ndani ya dakika 21 za kwanza….
Magoli matatu yamefungwa, Simba ikipenya kuingia 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank kwa kuifunga TMA Stars mabao 3-0 kwenye Dimba la KMC Complex. Magoli ya Simba yamefungwa na Valentine Nouma, Sixtus Sabilo kwa kujifunga na Lionel Ateba..... Kwa kuvuka hatua hii, Simba sasa itakutana na Bigman FC kwenye hatua hiyo...
HATTRICK: Steven Desse Mukwala amefunga hattrick, Simba ikiitandika Coastal Union mabao 3-0 kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid Arusha, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara. Mukwala amefunga magoli yote matatu dakika ya 30, 45 na 56 Tazama highlights...