Yanga SC imelipa kisasi kwa kuitandika Azam FC mabao 2-1 kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.... Yanga imepata mabao yake yote mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Pacome Zouzoua dakika 11 na Prince Dube dakika ya 34, huku Azam FC wakipata bao lao dakika ya 81. Tazama magoli....
KARIAKOO DERBY | Imepigwa dabi moja ya maana sana kwenye Dimba la Amaan, Zanzibar, Yanga na Simba wakimaliza dakika 90 bila bao, lakini burudani za kutosha. Hii ni mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania
Yanga SC imeichakaza JKT Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Wafungaji wa magoli haya ni Mohamed Hussein Zimbwe Jr,, Aurellio Depu, Mudathir Yahya, Prince Dube na Shekhan Ibrahim.
Ni mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA iliyopigwa kwenye Dimba la Al Salaam, Cairo nchini Misri, na timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars kuchwa 4-3 na Kuwait. Magoli ya Tanzania yamefungwa na M’mombwa 6’, 87’, na Taryin Allarakhia 34’ huku ya Kuwait yakitoka kwa Daham 46’, 52’ Nasser 63’ na Hamdan 69’
KMC vs SINGIDA BS: Kocha Marcio Maximo wa KMC, amesema mataifa ya Argentina na Brazil ni wapinzani ndani ya uwanja, ...
KARIAKOO DEEBY | Fahamu ukweli kuhusu matukio yote yaliyozua utata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba uliopigwa Septemba 16, 2025. Moja kati ya matukio yaliyozua gumzo ni goli pekee walilofunga Yanga na kuamua mshindi wa Ngao ya Jamii 2025. Osman Kazi na jopo lake wanamaliza utata kwa kutumia sheria na kanuni za soka
KUTOKA CAIRO MISRI: " ....msimu huu tunahitaji kuwapiku Yanga" Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wadi Degla FC inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo, Kocha wa Simba, Fadlu davids anaeleza baadhi ya mambo ambayo ameridhika nayo, na maeneo ambayo bado ana kazi ya kufanya.... Kuhusu kikosi chake, Kocha Fadlu anasema bado wanahitaji angalau mchezaji mmoja mwenye kitu cha ziada (X-Factor) atakayewaongezea kitu hasa kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mbio za ubingwa wa #NBCPremierLeague msimu ujao wakilenga kuwa juu ya Yanga ... Fadlu anasema anaamini mdhamini wao upande wa jezi, 'Jayruty', atalimaliza hilo.... Naye mfungaji wa moja kati ya magoli mawili ya Simba, Kibu Denis anazungumza machache kuhusu maendeleo ya kambi nchini Misri.... Patrick Nyembera anakuja na taarifa kamli kuhusu mchezo huo... #SimbaSC #SimbaEgypt #SimbaPreSeason
Yanga SC imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports, katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Dimba la Amahoro, jijini Kigali, Rwanda. Mchezo huo uliokuwa hitimisho la Siku ya Rayon Sports #RayonSportsDay , umeshuhudia wenyeji wakitangulia kwa goli la kujifunga kupitia kwa Aziz Andambwile. Yanga walicharuka na kupiga mabao matatu kupitia kwa Andy Boyeli, Pacome Zouzoua, na Bakari Mwamnyeto.
KUTOKA ISMAILIA: “Mwaka jana Fadlu alikuwa ni mgeni lakini mwaka huu ameshakuwa mwenyeji na ameshajua karibu wachezaji wote” Kocha msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola amesema ushindani ni mkubwa ndani ya kikosi hicho kwasababu kila mchezaji anataka kuonesha uwezo wake. Matola pia ametoa ratiba ya kikosi hicho watakapofika jijini Cairo. Mchezaji Saleh Karabaka anasema kuingia kwenye maji yenye barafu ni shughuli nzito kwake, ni lazima pawepo watu watatu kumshika. Wachezaji wengine waliozungumzia maendeleo ya kambi hiyo ni pamoja na Bajaber Mohamed, Morice Abraham pamoja na Hussein Abel ambaye amefichua namna wachezaji ‘walivyoamka’ kambini. #Simba