MZIZIMA DERBY | Ni sare ya 2-2 kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC, uliopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Azam wametangulia kwa goli la Gibril Sillah dakika ya 01, kabla ya Elie Mpanzu kusawazisha dakika ya 25 na Abdulrazak Hamza kuongeza la pili dakika ya 76. Nyota wa mchezo ni ‘Super Sub’, Zidane Sereri ndiye aliyeweka mambo sawa kwa kuifungia Azam FC bao la kusawazisha dakika ya 88, kwa assist ya aina yake kutoka kwa Feisal Salum Feitoto.
Clatous Chama amefunga magoli mawili, Yanga ikiichakaza Mashujaa FC magoli 5-0 kwenye Dimba la Lake Tanganyika, Kigoma, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.... Chama amefunga dakika ya 74 na 83 huku mengine yakifungwa na Duke Abuya, Prince Dube na Khalid Aucho..
Zimepigwa penati tatu, Simba ikiitandika Namungo FC mabao 3-0 kwenye Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Jean Charles Ahoua amefunga penati mbili, huku Lionel Ateba akikosa penati moja iliyookolewa na golikipa wa Namungo, Jonathan Nahimana. Goli la tatu kwa Simba limefungwa na Steven Mukwala dakika za majeruhi... Katika mchezo huu pia, Namungo wamepata pigo baada ya beki wake Derrick Mukombozi kutolewa kwa kadi nyekundu...
Yanga SC imeendeleza ubabe kwenye ligi, kwa kumchapa Singida Black Stars mabao 2-1 kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Waliofunga magoli ya Yanga ni Clement Mzize dakika ya 14 na Prince Dube dakika ya 43 wakati Jonathan Sowah akifunga goli pekee la kufutia machozi... Hii ni Ligi Kuu ya NBC #NBCPremierLeague
Stephane Aziz Ki amefunga #hattrick ... Yanga ikiitandika KMC mabao 6-1 kwenye dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya NBC. Hat-trick ya Aziz Ki imepatikana kwa penati mbili dakika za 18 na 56, huku lingine lingia nyavuni dakika ya 49. Aliyefungua mlango wa magoli ni Prince Dube dakika ya 10... huku Maxi Nzengeli na Israel Mwenda nao wakifunga dakika za majeruhi... Bao la kufutia machozi limetoka kwa Redemtus Mussa dakika ya 51. Haya hapa magoli yote...
Magoli matatu yote kipindi cha kwanza… Simba inaipiga Tanzania Prisons 3-0 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam. Wafungaji ni Jean Charles Ahoua, Elie Mpanzu na Ladack Chasambi. Hii ni Ligi Kuu ya NBC 2024-25
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya NBC Premier League kati Tabora United dhidi ya Simba SC. Simba imeshinda kwa jumla ya magoli 3-0, Magoli yamefungwa na Leonel Ateba na Shomari Kapombe
#MakarashaDay: Tazama ‘vimbwanga’ vya Bernard Morrison baada ya kutambulishwa ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya ikiwa ni ingizo jipya kwenye kikosi cha KenGold. Wchezaji wengine waliotambulishwa ni pamoja na Morrison ni Kelvin Yondani na Obrey Chirwa. #MakarashaDay #KenGold #HashukiMtu #AzamSports1HD