Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara Simba SC wamepoteza mchezo wa pili kwenye ligi hiyo msimu huu kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera ‘wamewapoteza’ Simba kipindi cha kwanza kwa kuonesha kandanda safi na kufanikiwa kupata mabao mawili yakifungwa na Kassim Khamis dakika ya 18 na Ramadhan Kapera dakika 41. Simba walifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Haruna Niyonzima na James Kotei nafasi zao zikichukuliwa na John Bocco na Hassan Dilunga, mabadiliko ambayo yaliwasaidia kupata bao moja likifungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 64. Ushindi wa Kagera Sugar dhidi ya Simba SC leo umeibeba kutoka nafasi ya 17 hadi nafasi ya 13 baada ya kufikisha pointi 39 huku Simba ikiendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu na pointi 60.
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars FT: Kagera Sugar 2-1 Simba Uwanja: Kaitaba Gooooal Emmanuel Okwi dk ya 63 Kipindi cha pili kimeanza, Zimeongezwa dakika 5 Goooooal: Kassim Khamis Goooooal: Ramadhan Kapera Zinaongezwa dakika nne Hasan Dilunga njano dk ya 67 Okwi dk ya 64 njano Said Kipao wa Kagra Sugar anaonyeshwa kadi ya njano dk ya 69, Kassim njano dk ya 73. KASSIM Khamis anawanyanyua mashabiki wa Kagera Sugar dakika ya 20 kwa kuitanguliza timu yake kuongoza mbele ya Simba akimalizia pasi ya Ramadhan Kapera. Dakika ya 40 Kagera Sugar wanapachika bao la pili kupitia kwa Ramadhan Kapera. Kagera Sugar iliyo chini ya kocha Mecky Maxime imeanza kwa kasi kushambulia lango la Aish Manula na kupata kile ambacho ilikuwa inahitai kwa sasa. Emmanuel Okwi anaandika bao la kwanza kwa Simba dakika ya 63 akimalizia pasi ya Chama. Mashabiki waliojitokeza ni wengi kuona namna ushindani ulivyo huku mashambulizi kwa timu zote yakiwa ni makali. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
Shabiki wa Klabu ya Soka ya Simba Bwana Ramadhan Mohamed ambaye alikwenda Dar es Salaam akitokea Jijini Mbeya kwa miguu ili ashuhudie mchezo wa robo fainali ya #CAFCL kati ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe kutoka DRC, leo amekutana na viongozi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na sekretarieti ya Klabu ya Soka ya Simba ambapo amehaidiwa kugharamiwa na klabu ya Simba kwenda Lubumbashi nchini DRC, kwaajili ya kuangalia mchezo wa marudiano kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba SC ambao utachezwa Jumamosi hii. #NguvuMoja #SimbaSc #YesWeCan #HajiManara
Mabao mawili ya Adam Adam yameipa Tanzania Prisons ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Wenyeji Lyon ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa Ramadhan Chombo Redondo, lakini Adam akaisawazishia Prisons dakika ya 51 na kuifungia bao la ushindi dakika ya 69. Haya hapa mabao yote.
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA 1-0 AL AHLY Dakika 90 zinamalizika Simba 1-0 Al Ahly Uwanja wa Taifa na Simba wanavuna pointi tatu nyumbani. Dakika ya 90+4 Simba wanapata kona Dakika ya 90 + 3 Kagere anadondoka, mpira unaendelea Dakika ya 90 Kotei anatolewa nje akiwa ameumia anaingia Mzamiru Yassin Dakika ya 90 Waarabu wanapaisha mpira mawinguni wakiwa eneo la hatari. Dakika nne zinaongezwa Taifa, Simba wameacha kukaba Dakika ya 90 mwarabu anakosa bao la wazi Dakika ya 89 Kotei anapiga mpira nje kwa waarabu Dakika ya 87 Manula anaamka na mpira unaanza kwenda kwa Waarabu. Dakika ya 85 Manula alikwenda hewani wakati anashuka anaangukia mgongo. Dakika ya 84 Simba wanaanza mashambulizi kwenda kwa Mwarabu, Mpira unatolewa nje anarusha Zimbwe, Kagere, wanadaka Waarabu. Dakika ya 83 Mkude anauza kwa waarabu. Dakika ya 82 Waarabu wanapata faulo inachezwa vizuri ila kichwa cha Mwarabu kinapaa Mawinguni. Dakika ya 81 Bocco anatolewa nafasi yake inachukuliwa na Dilunga. Dakika ya 81 Chama anapoteza Mpira kwa waarabu wanaanza safari kwa Manula sasa, Juuko anacheza rafu Dakika ya 80 Manula ananyanyuka, Waarabu wanaanza safari kumfuata sasa. Dakika ya 79 bado Manula anagangwagangwa Uwanjani. Dakika ya 77 Zana anakaba,ila bado waarabu wanamuwinda Manula anaokoa baada ya mabeki kukabia kwa macho na kumuumiza Manula. Dakika ya 76 Kagere alipata pasi kutoka kwa Kotei akapaisha mpira mawinguni. Dakika ya 75 Waarabu wanamchezea rafu Kotei Dakika ya 75 bado waarabu wapo kwa mshikaji Manula Dakika ya 74 waarabu wanaanza safari kwenda kwa Manula wao karibu na eneo la hatar sasa Dakika ya 73 waarabu wanaanza safari kwa Manula Dakika ya 72 Kotei anacheza rafu kwa waarabu wanapata faulo haziai matunda. Dakika ya 71 Okwi anarejea Uwanjani kuwavaa waarabu. Dakika ya 69 Okwi anatolewa akiwa kwenye machela. Dakika ya 67, Mkude, Bocco mchezaji wa Simba anapata majeraha dakika ya 68 Okwi baada ya kuanguka na kupoteza fahamu kwa muda wa dakika kadhaa. Dakika ya 66 Chama anatoa Mpira nje Dakika ya 64 Kagere anaandika bao tamu na kumyayua Mohamed 'Mo' akitumia pasi ya Bocco ya kifua baada ya kupokea pasi ya mmwaga maji Zana. Dakika ya 63 Waarabu wanamfuata Manula , Wawa anaanua hatari. Dakika ya 62 Bocco anatoa Boko akiwa eneo la hatari baada ya kupewa pasi na Okwi Dakika ya 61 Simba wanarusha kwa kumtumia Mohamed Dakika ya 60 Zana aliingiza majaro ya hatari eneo la hatari ila mira ukababatizwa ukatoka nje goal kick. Dakika ya 59 Juuko anapoteza kwa waarabu, Wawa anafanya yake, Chama, Kagere anapoteza. Dakika ya 58 Mkude anamsumbua Mwarabu na kumchezea faulo. Dakika 90 zinamaliizika Simba 1-0 Al Ahly Dakika ya 90+4 Simba wanapata kona Dakika ya 90 + 3 Kagere anadondoka, mpira unaendelea Dakika ya 90 Kotei anatolewa nje akiwa ameumia anaingia Mzamiru Yassin Dakika ya 90 Waarabu wanapaisha mpira mawinguni wakiwa eneo la hatari. Dakika nne zinaongezwa Taifa, Simba wameacha kukaba Dakika ya 90 mwarabu anakosa bao la wazi Dakika ya 89 Kotei anapiga mpira nje kwa waarabu Dakika ya 88 Waarabu wanaanza safari kwa Manula baada ya Dilunga kucheza faulo. Dakika ya 57 Waarabu wanaanza safari kwa Manula Juuko anaanua Dakika ya 57 Wawa anauza kwa waarabu. Dakika ya 56 Juuko Murshid anagangwa gangwa guu lake la kushoto. Dakika ya 55 Okwi anamchezea faulo Mwarabu karibu na eneo la hatari, Waarabu wanatumia nafasi ila mpira unapaa mawinguni. Dakika ya 54 Zana anauza kwa Waarabu Dakika ya 53 waarabu wanaanza safari kwenda kwa Manula, wanarejea nyumbani kisha wanaendela kupitia kwa Mohamed, Ramadhan, Khalid, Junior Wawa anazuia. Dakika ya 52 Kager anashindwa kutumia nafasi ya mpira wa Zana. Dakika ya 51 Waarabu wanapata faulo na mlinda mlango wao anapata hudua ya kwanza. Kikosi cha Simba kitakachocheza mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly: Aishi Manunula, Zaha Coulibaly, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Clstous Chama, Jonas Mkude, John Mkude, John Bocco, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
Goli la dakika ya mwisho ya mchezo limeiokoa Mtibwa Sugar kwa kuipa sare ya bao 1-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa manungu Complex, mkoani Morogoro. Bao hilo la kusawazisha limefungwa na Jaffary Salum Kibaya akimalizia kwa kichwa kona iliyochongwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ baada ya wageni katika mchezo huo African Lyon kutangulia kupata bao dakika ya 62 kupitia kwa mkongwe Ramadhan Chombo Redondo. Matokeo hayo yameipandisha Mtibwa kutoka nafasi ya 13 hadi nafasi ya 10 ikifikisha pointi 30 katika michezo 21 huku African Lyon ikiendelea kusalia mkiani na licha ya kufikisha pointi 20 baada ya kucheza michezo 25.
Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali.
Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali. Mchezo huo ulikuwa na kasi sana, Azam FC ikianza kwa mashambulizi makali langoni mwa Alliance, ambapo dakika ya kwanza Obrey Chirwa, alikosa bao la wazi baada ya kuupiga vibaya mpira akiwa anatazamana na lango ndani ya eneo la hatari, akipokea pasi ya Donald Ngoma. Mabingwa hao waliweza kupata ugumu kuipenya safu ya ulinzi ya Alliance, kutokana na timu hiyo kusimama wengi kujilinda nyuma ya mpira wakati Azam FC ikishambulia. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, kipa wa Azam FC, Razak Abalora, alioneshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano iliyosababishwa na lugha ya kutoridhishwa na maamuzi aliyoitoa kwa mwamuzi huyo. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 48 katika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ikizidiwa pointi saba na kinara Yanga aliyefikisha 55 kufuatia suluhu yake ya jana dhidi ya Singida United.