MASHABIKI SIMBA "TULIJUA Yatatokea Matokeo Haya /TUNA Imani na Simba"
MASHABIKI SIMBA "TULIJUA Yatatokea Matokeo Haya /TUNA Imani na Simba"

MASHABIKI SIMBA "TULIJUA Yatatokea Matokeo Haya /TUNA Imani na Simba" MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Coastal Union na Simba uliochezwa leo, Julai 23 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga umekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu bila kufungana ndani ya dakika 90. Coastal Union inayonolewa na Juma Mgunda ililiandama lango la Simba kipindi cha pili kwa kumtumia mtupiaji wao namba moja Ayoub Lyanga mwenye mabao nane ndani ya ligi ila mikono ya Beno Kakolanya iliokoa hatari zake. Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck ilikuwa ikifanya mashambulizi kwa kumtumia Meddie Kagere na John Bocco mambo yalikuwa magumu kwao. Bocco alitolewa kipindi cha pili nafasi yake ikachukuliwa na Clatous Chama na Miraj Athuman alitolewa ia nafasi yake ikachukuliwa na Deo Kanda ila ngome ya Coastal Union chini ya Bakari Nondo ilibaki kuwa imara. Pascal Wawa alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa leo baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano hivyo Simba ilimaliza dakika tisini ikiwa na wachezaji 10 baada ya beki huyo wa kigeni kutolewa dakika ya 75. Atakuwa akiwashuhudia wenzake kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Polisi Tanzania, Ushirika, Moshi. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 85 baada ya kucheza mechi 37, Coastal Union inafikisha jumla ya pointi 53 zote zinauhakika wa kubaki ndani ya ligi. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT AMAZON: https://www.amazon.com/shop/globaltvonline ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982), ( +255 713 837506) ⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ HABARI MPYA DAILY:shorturl.at/mnux2 ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua ⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews ⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline



Kocha Polisi Tanzania akiri kuzidiwa na Ndanda licha ya ushindi wa 1-0. Tazama goli la penati
Kocha Polisi Tanzania akiri kuzidiwa na Ndanda licha ya ushindi wa 1-0. Tazama goli la penati

Goli la penati kutoka kwa Marcel Kaheza lililowapa Polisi Tanzania pointi tatu dhidi Ndanda SC kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi. Kocha wa Polisi Malale Hamsini akiri kuzidiwa licha ya ushindi. FT: Polisi Tanzania 1-0 Ndanda SC #LigiKuuTanzaniaBara #VodacomPremierLeague #VPLUpdates #VPL #PolisiTanzania #NdandaSC Tazama Vodacom Premier League, taarifa ya Habari na vipindi vingine vya Habari na Matukio LIVE kutoka Azam TV na UTV kupitia Azam TV Decoder au AzamTV Max App. Unaweza kupata AzamTV Max App kwa ajili ya Android kutoka hapa: ► https://bit.ly/2wB6zmR Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz



( VPL) USHIRIKA MOSHI
( VPL) USHIRIKA MOSHI

#2gendah24tvonline#Polisitz#Yangasc#Moshi#Morrison #LIVE POLISI TANZANIA Vs. YANGA SC ( VPL) USHIRIKA MOSHI LIKE AND SHARE



Alichokisema Kocha Wa Kariobangi Kuwafunga Yanga Sport Pesa
Alichokisema Kocha Wa Kariobangi Kuwafunga Yanga Sport Pesa

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars KIKOSI cha Yanga, leo kimepoteza mchezo wake wa kombe la SportPesa ikiwa ni hatua ya robo fainali kwa kukubali kufungwa mabao 3-2 dhidi ya KK Sharks ya Kenya mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa. Michuano ya SportPesa Cup ambayo kwa sasa ni msimu wake wa tatu imeshirikisha timu nane ikiwa ni nne kutoka Tanzania ambazo ni Singida United, Simba, Mbao na Yanga na zile za kutoka Kenya ni pamoja na KK Sharks, Bandari, AFC Leopards na Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi. Kipindi cha kwanza Yanga walikubali kupoteza kutokana na uzembe wa mabeki ambapo dakika ya 9 KK Sharks waliandika bao la kwanza kupitia kwa Abuye Duke na baada ya kuzidisha mashambulizi wakaandika bao la pili dakika ya 37 kupitia kwa Abege George. Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika Yanga walikuwa nyuma kwa mabao mawili, kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko kwa kumtoa Haruna Moshi na kuingia Amiss Tambwe pamoja na Abdallah Shaibu na kuingia Thaban Kamusoko, Mrisho Ngassa nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke pamoja na Paul Godfery nafasi yake kuchukuliwa na Juma Abdul kasi ya Yanga ilianza kuonekana. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars/ Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars/ Twitter: https://twitter.com/kidanistars



KURASA ZA MWISHO 15/12/2018: Usajili wa Yanga na mechi ya Simba vs Nkana zafunika magazeti
KURASA ZA MWISHO 15/12/2018: Usajili wa Yanga na mechi ya Simba vs Nkana zafunika magazeti

Kuna mwengi yametikisa michezoni wiki hii lakini kurasa za mwisho za magazeti ambazo huandika habari za michezo, zimetoa kipaumbele zaidi kwa habari ya usajili ndani ya klabu ya Yanga, ambao wametumia dirisha dogo kumnasa kiungo Haruna Moshi Boban. Taarifa nyingine iliyopewa uzito ni kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Nkana FC dhidi ya Simba SC unaopigwa leo Desemba 15, 2018 nchini Zambia. Ndani ya Studio Philip Cyprian yuko na wanahabari nguli wa michezo, wanafanya uchambuzi na mjadala kuhusu yaliyopewa uzito kwenye kurasa hizo. Vilevile tumetembelea vibanda vya magazeti na kuzungumza na wafuatiliaji wa habari za michezo magazetini, wengi wakiwa ni mashabiki wa soka. Kipindi hiki ni kila Jumamosi saa 3:30 asubuhi Azam Sports 2.



HIGHLIGHTS: ALLIANCE FC 1-1 AFRICAN LYON (TPL 27/08/2018)
HIGHLIGHTS: ALLIANCE FC 1-1 AFRICAN LYON (TPL 27/08/2018)

Timu ya Alliance FC ya Jijini Mwanza imebanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na African Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo CCM Kirumba Jijini Mwanza. Mkongwe, Haruna Moshi 'Boban' ndiye aliyetanguliza African Lyon kwa bao la dakika ya 8 kazi nzuri ikifanywa na Victor Da Costa. Baada ya mshambulizi ya muda mrefu hatimaye Michael Chinedu aliyeingia kutoka benchi aliipa kashikashi safu ya ulinzi ya African Lyon na kuisawazishia timu yake ya Alliance FC dakika za nyongeza. Hata hivyo dakika ya 78 ya mchezo, Alliance walikwamisha mpira nyavuni lakini haikuwa bao ikionekana kuwa kuna faulo ilifanyika kabla yay a bao hilo.



Goli la Haruna Moshi ‘Boban’: Alliance vs African Lyon (TPL 27/08/2018)
Goli la Haruna Moshi ‘Boban’: Alliance vs African Lyon (TPL 27/08/2018)

Mkongwe, Haruna Moshi 'Boban' anaitanguliza African Lyon dhidi ya Alliance kwenye dimba la CCM Kirumba, kazi nzuri ikifanywa na Victor Da Costa. Ni mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.




« Previous


Popular Tags

#Michael Jordan  #Chris Paul  #Cleveland Cavaliers  #Counter Attack Goals Football  #Shaquille O'Neal  #Zlatan Ibrahimovi  #Lionel Messi  #Goalkeeper Saves  #Gareth Bale  #Lionel Messi  

Popular Users

#LilTunechi  #JohnCena  #billsimmons  #WWE  #AntDavis23  #DeAndre  #ddlovato  #geniebouchard  #neymarjr  #Ky1eLong  #SHAQ  #RealSkipBayless  #josecanseco  #THNRyanKennedy