Timu ya Alliance FC ya Jijini Mwanza imebanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na African Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo CCM Kirumba Jijini Mwanza. Mkongwe, Haruna Moshi 'Boban' ndiye aliyetanguliza African Lyon kwa bao la dakika ya 8 kazi nzuri ikifanywa na Victor Da Costa. Baada ya mshambulizi ya muda mrefu hatimaye Michael Chinedu aliyeingia kutoka benchi aliipa kashikashi safu ya ulinzi ya African Lyon na kuisawazishia timu yake ya Alliance FC dakika za nyongeza. Hata hivyo dakika ya 78 ya mchezo, Alliance walikwamisha mpira nyavuni lakini haikuwa bao ikionekana kuwa kuna faulo ilifanyika kabla yay a bao hilo.
MZIZIMA DERBY | Magoli mawili, moja likiwa ni la kujifunga kupitia kwa Nathan Fasika Idumba na Clatous Chama yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC, katika #MzizimaDerby ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.
YANGA DAY: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga SC dhidi ya Aigles du Congo. Goli la Yanga limefungwa na Peter Shalulile na magoli ya Aigles du Congo yamefungwa na Talasy Tonny. FT: Yanga SC 1-2 Aigles du Congo #YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
SIMBA DAY: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya kirafiki kati ya Simba SC dhidi ya Kenya Police Goli limefungwa na Elvis Rupia. FT: Simba SC 0-1 Police Kenya #SimbaDay #SimbaSC #Miaka90 #MechiYaKirafiki #SimbaSC #KenyaPolice
SIMBA DAY: Eba hii kali…Semaji Ahmed Ally aingia na simba wawili wa porini…Kila mtu abaki mdomo wazi. Neno moja tu kwa semaji Ni shamrashamra za #SimbaDay #SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
Fuatilia uchambuzi na mengi yaliyojiri dimbani baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba vs Yanga uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Ndani ya studio Patrick Nyembera akiwa na wachambuzi Abissay Stephen na Godlisten Maro. Matangazo yako LIVE #AzamSports1HD lakini unaweza pia kuitazama kupitia katika #AzamTVMaxApp ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz
Simba SC imekabwa koo na kulazimishwa suluhu na Mogadishu City Club ya Somalia, katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Kagame 2026, ukipigwa kwenye Dimba la Kigali, Rwanga. Kwenye mchezo huu Simba imewatumia baadhi ay nyota wake wapya akiwemo Ibrahim Doumbia , Cooper, Kelvin Nashon na wengine. Tazama highlights.