Timu ya Alliance FC ya Jijini Mwanza imebanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na African Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo CCM Kirumba Jijini Mwanza. Mkongwe, Haruna Moshi 'Boban' ndiye aliyetanguliza African Lyon kwa bao la dakika ya 8 kazi nzuri ikifanywa na Victor Da Costa. Baada ya mshambulizi ya muda mrefu hatimaye Michael Chinedu aliyeingia kutoka benchi aliipa kashikashi safu ya ulinzi ya African Lyon na kuisawazishia timu yake ya Alliance FC dakika za nyongeza. Hata hivyo dakika ya 78 ya mchezo, Alliance walikwamisha mpira nyavuni lakini haikuwa bao ikionekana kuwa kuna faulo ilifanyika kabla yay a bao hilo.