Magoli Yote: SIMBA 5 -1 ALLIANCE FC, LIGI KUU, 24 OKT 2018
Magoli Yote: SIMBA 5 -1 ALLIANCE FC, LIGI KUU, 24 OKT 2018

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars OKWI, CHAMA, KWASI NA SALAMBA WOTE WAFUNGA SIMBA SC YAIKANDAMIZA ALLIANCE FC 5-1 TAIFA MABINGWA watetezi, #SimbaSC wamepata ushindi wa kishindo baada ya kuichapa 5-1 #AllianceFC katika mchezo wa #LigiKuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikiziwa pointi nne na vinara, Azam FC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi. Watani wao wa jadi, Yanga SC wanafuatia kwa pointi zao 19 na kesho watacheza mechi yao ya nane kwa kumenyana na KMC Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa. Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi alifunga bao la kwanza dakika ya 10 kwa kichwa akimalizia pasi ya kocha baada ya krosi ya beki Mghana, Nicholas Gyan baada ya kona fupi kutoka upande wa kulia. Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan/Shomari Kapombe dk46, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Pascal Wawa, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Hassan Dilunga dk61, Clatous Chama, Adam Salamba/Meddie Kagere dk75, John Bocco na Emmanuel Okwi. Alliance FC; Kelvin Richard, Israle Patrick, Hance Masoud, Wema Sadock, Geoffrey Luseke, Juma Nyangi, Dickson Ambundo, Balama Mapinduzi/Martin Kiggi dk89, Michael Chinedu/Juhudi Philemon dk61, Jamal Mtegeta/Zabona Khamis dk80 na Siraj Juma. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars



HIGHLIGHTS: SIMBA SC 2-1 MTIBWA SUGAR (NGAO YA JAMII 2018)
HIGHLIGHTS: SIMBA SC 2-1 MTIBWA SUGAR (NGAO YA JAMII 2018)

Timu ya Simba SC imefanikiwa kuibuka na ubingwa taji la Ngao ya Jamii mwaka 2018 baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1. Mchezo huo wa unaoashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2018/19 umepigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza, leo Agosti 18, 2018. Magoli yote matatu yamepatikana katika kipindi cha kwanza, Simba ikitangulia kwa bao la Meddie Kagere dakika ya 29 likisawazishwa na Kelvin Kongwe Sabato dakika ya 33, huku Hassan Dilunga akiifungia Simba bao la pili na la ushindi.



NJOMBE MJI 0 - 1 MTIBWA SUGAR: Goli la Hassan Dilunga lililoipeleka Njombe Mji 'kuchungulia kaburi'
NJOMBE MJI 0 - 1 MTIBWA SUGAR: Goli la Hassan Dilunga lililoipeleka Njombe Mji 'kuchungulia kaburi'

Mchezo wa Njombe Mji na Mtibwa Sugar umemalizika kwa Mtibwa Sugar kuibuka na ushindi wa bao 1 huku bao hilo likiipeleka Njombe Mji 'mlangoni' akichungulia kaburi la kurejea daraja la kwanza.



Magoli ya Mtibwa Sugar ikiichapa Stand United 2-0 na kutinga fainali ya ASFC
Magoli ya Mtibwa Sugar ikiichapa Stand United 2-0 na kutinga fainali ya ASFC

Mtibwa Sugar ya Morogoro, imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Stand United katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) uliopigwa leo kwenye dimba la Kambarage, Shinyanga. Mabao yote ya Mtibwa yamefungwa na Hassan Dilunga.



SINGIDA UNITED 0-3 MTIBWA SUGAR, VPL HIGHLIGHTS (06/04/2018)
SINGIDA UNITED 0-3 MTIBWA SUGAR, VPL HIGHLIGHTS (06/04/2018)

Katika mchezo huo uliokuwa mbashara Azam Sports 2, Mtibwa Sugar ikiwa katika ubora wake, imeitandika Singida United magoli 3-0. Magoli ya Mtibwa yamefungwa na Kelvin Sabato ‘Kiduku’ aliyefunga goli la kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo (free kick) dakika ya 22 ya mchezo na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Mtibwa walikuwa mbele kwa bao hilo. Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kuzidisha moto langoni kwa Singida na hatimaye kupata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Salum Kihimbwa akimlizia pasi ya Hassan Dilunga, huku Dilunga mwenyewe akiweka wavuni bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 71.




« Previous


Popular Tags

#Sergio Aguero  #Counter Attack Goals Football  #Best Goals  #Chicago Bulls  #Best Ball Controls  #Philadelphia 76ers  #Anthony Davis  #Shot Goals  #Zlatan Ibrahimovi  #Best Goals  

Popular Users

#TheEllenShow  #narendramodi  #KevinHart4real  #britneyspears  #JayBilas  #DjokerNole  #wizkhalifa  #BBCBreaking  #richarddeitsch  #realmadrid  #TheNotoriousMMA  #iamsrk  #StephenCurry30  #JoelEmbiid