Azam TV's user profile page. Match highlights, posts and more on site!

“”

 Report User

Latest Posts

Rayon Sports 1-3 Yanga SC | Highlights | Mechi ya Kirafiki | Rayon Sports Day 15/08/2025
Rayon Sports 1-3 Yanga SC | Highlights | Mechi ya Kirafiki | Rayon Sports Day 15/08/2025

Yanga SC imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports, katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Dimba la Amahoro, jijini Kigali, Rwanda. Mchezo huo uliokuwa hitimisho la Siku ya Rayon Sports #RayonSportsDay , umeshuhudia wenyeji wakitangulia kwa goli la kujifunga kupitia kwa Aziz Andambwile. Yanga walicharuka na kupiga mabao matatu kupitia kwa Andy Boyeli, Pacome Zouzoua, na Bakari Mwamnyeto.



Kocha Msaidizi Simba SC, Matola atoa ratiba ya kikosi hicho, Abel afichua siri ya kambi
Kocha Msaidizi Simba SC, Matola atoa ratiba ya kikosi hicho, Abel afichua siri ya kambi

KUTOKA ISMAILIA: “Mwaka jana Fadlu alikuwa ni mgeni lakini mwaka huu ameshakuwa mwenyeji na ameshajua karibu wachezaji wote” Kocha msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola amesema ushindani ni mkubwa ndani ya kikosi hicho kwasababu kila mchezaji anataka kuonesha uwezo wake. Matola pia ametoa ratiba ya kikosi hicho watakapofika jijini Cairo. Mchezaji Saleh Karabaka anasema kuingia kwenye maji yenye barafu ni shughuli nzito kwake, ni lazima pawepo watu watatu kumshika. Wachezaji wengine waliozungumzia maendeleo ya kambi hiyo ni pamoja na Bajaber Mohamed, Morice Abraham pamoja na Hussein Abel ambaye amefichua namna wachezaji ‘walivyoamka’ kambini. #Simba



Simba yaichapa Carabat FC 2-0, Bajaber, Sowah wacheka na nyavu
Simba yaichapa Carabat FC 2-0, Bajaber, Sowah wacheka na nyavu

KUTOKA MISRI: Kikosi cha Simba kilichopo Misri, katika maandalizi ya msimu mpya wa NBC Premier League na mashindano ya kimataifa, kimecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Carabat FC, ambapo Mnyama ameshinda magoli 2-0. Goli la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Mohammed Bajaber huku goli la pili likifugwa kipindi cha pili na Jonathan Sowah. Wachezaji wote wawili wamesajiliwa msimu huu. #Simba #KambiYaSimba



SIMBA SC: Elie Mpanzu aanza 'tizi' kambini Misri ; Meneja Simba amaliza utata kuhusu uhalali wake
SIMBA SC: Elie Mpanzu aanza 'tizi' kambini Misri ; Meneja Simba amaliza utata kuhusu uhalali wake

KUTOKA MISRI | “….hakuna kiumbe yeyote anayeweza kujiita Eliiiii zaidi ya Simba SC” Kikosi cha Simba SC kikiwa kambini nchini Misri, jioni ya leo kimepiga tizi lililomuhusisha pia kiungo wao Elie Mpanzu ambaye ameripoti kambini hapo leo… Katika tizi hizo hilo, meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyemamu amefafanua machache kuhusu utata uliokuwepo juu ya mchezaji huyo, akisema “…ni propaganda…ni Gen-z ambao wameingia kwenye mfumo wa kisasa wa mpira” Rweyemamu amesema klabu hiyo haiwezi kufanya makosa ya kumsajili mchezaji wa aina hiyo kwa mkataba wa miezi sita na kusisitiza kuwa “…Elie Mpanzu yupo, na ataendelea kuwepo hadi Simba itakavyoamua vinginevyo



Highlights | Tanzania 1-0 Uganda | CECAFA 3 Nations Tounarment 22/07/2025
Highlights | Tanzania 1-0 Uganda | CECAFA 3 Nations Tounarment 22/07/2025

Goli pekee la Idd Selemani 'Nado' limeipa Tanzania #TaifaStars pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda, katika mchezo wa ufunguzi wa michuano maalum ya CECAFA 3 Nations Tounarment #CECAFA3NT inayopigwa kwenye Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha...



Yanga yatoa siri jinsi ilivyomnasa kiungo Moussa Balla Conte
Yanga yatoa siri jinsi ilivyomnasa kiungo Moussa Balla Conte

“…tuliweka kiwango kizuri cha fedha kumshawishi mchezaji na klkabu yake” Nneno la Ally Kamwe kuhusu usajili wa kiungo Moussa Balla Conte ambaye leo ametua rasmi Jangwani kwa mkataba wa miaka mitatu… Kamwe ameeleza jinsi ilivyokuwa ngumu kumpata na jinsi walivyoweza kumshawishi yeye na klabu yake licha ya kuwa na ofa nyingi….. Kuhusu hatma ya Khalid Aucho, Kamwe amesema majibu yatatoka Julai 20 baada ya kupokea ripoti ya CEO wa klabu hiyo… Mwisho, Ally Kamwe anatoa ujumbe kwa walioumizwa na usajili huo akiomba kusajiliwa na timu inayohitaji mchezaji mwenye jina la Conte…. #YangaSC #Usajili #BallaConte



Yanga SC 2-0 Simba SC | Highlights | Kariakoo Derby | NBC PL 25/06/2025
Yanga SC 2-0 Simba SC | Highlights | Kariakoo Derby | NBC PL 25/06/2025

KARIAKOO DERBY | Magoli ya Pacome Zouzoua kwa penati na Clement Mzize yameipa Yanga pointi tatu muhimu dhidi ya mtani wake Simba SC na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2024/25 baada ya kufikisha alama 82 dhidi ya 78 za Simba... Huu ulikuwa ni mchezo wa mwisho wa msimu ambao pia ulikuwa ukisubiriwa kutoa maamuzi ya nani awe bingwa wa ligi hii msimu huu... Mbungi imepigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.



Highlights

Magoli | Fountain Gate Princess 2-1 Bunda Queens | Singida BIG Day - 02/08/2023
Magoli | Fountain Gate Princess 2-1 Bunda Queens | Singida BIG Day - 02/08/2023

Tazama magoli yote matatu yaliyowekwa nyavuni kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Fountain Gate Princess dhidi ya Bunda ...



MSHIKEMSHIKE VIWANJANI - 24/07/2023
MSHIKEMSHIKE VIWANJANI - 24/07/2023

Tazama habari mbalimbali za michezo zilivyojiri hii leo kwenye viunga vya kimichezo ikiwa kubwa zaidi ni Simba SC imecheza ...



WIKI YA MWANANCHI | Kosakosa za mechi kati ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs - 22/07/2023
WIKI YA MWANANCHI | Kosakosa za mechi kati ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs - 22/07/2023

WIKI YA MWANANCHI: Tazama kosakosa za hatari zilifanywa kwenye mechi ya kirafiki kati ya Yanga SC dhidi ya Kaizer Chiefs ...



Yanga SC 1-0 Kaizer Chiefs | Highlights | Friendly Match - 22/07/2023
Yanga SC 1-0 Kaizer Chiefs | Highlights | Friendly Match - 22/07/2023

Highlights: hapa chuma cha Kennedy Musonda assist saafi kutoka kwa Maxi Mpia akiwaadhibu Kaizer Chiefs kwenye mechi ya ...



Goli la Yanga SC 1-0 Kaizer Chiefs | Mechi ya Kirafiki - 22/07/2023
Goli la Yanga SC 1-0 Kaizer Chiefs | Mechi ya Kirafiki - 22/07/2023

hapa chuma cha Kennedy Musonda assist saafi kutoka kwa Maxi Mpia akiwaadhibu Kaizer Chiefs kwenye mechi ya kirafiki ...



Magoli | Yanga 1-1 Polisi Tanzania | U20 Premier League 26/06/2023
Magoli | Yanga 1-1 Polisi Tanzania | U20 Premier League 26/06/2023

Yanga U20 na Polisi Tanzania U20 wametoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 , mchezo wa mwisho wa kundi katika Ligi Kuu ya ...



Magoli | Mbeya City 2-1 Namungo | U20 Premier League 25/06/2023
Magoli | Mbeya City 2-1 Namungo | U20 Premier League 25/06/2023

Timu ya vijana ya Mbeya City U20 imepata ushindi wa pili kwa kuitandika Namungo U20 mabao 2-1 katika muendelezo wa Ligi ...



Highlights | Mbeya City 0-1 Mashujaa FC | Play-Off 2nd Leg - 24/06/2023
Highlights | Mbeya City 0-1 Mashujaa FC | Play-Off 2nd Leg - 24/06/2023

Mashujaa FC ya Kigoma imepanda daraja kucheza ligi kuu ya NBC msimu ujao kwa kuichapa na kuishusha daraja Mbeya City ...




« Previous Next »


User Detail Page

You can find user latest posts and related content on the page. Friends, comments for events / matches are also available on the page. Even you can find users who are same pleasure with current user.

#Travel, #SupportYourTeam, #AllAboutSports