KUTOKA MISRI: Kikosi cha Simba kilichopo Misri, katika maandalizi ya msimu mpya wa NBC Premier League na mashindano ya kimataifa, kimecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Carabat FC, ambapo Mnyama ameshinda magoli 2-0. Goli la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Mohammed Bajaber huku goli la pili likifugwa kipindi cha pili na Jonathan Sowah. Wachezaji wote wawili wamesajiliwa msimu huu. #Simba #KambiYaSimba