Content removal request!


Kocha Msaidizi Simba SC, Matola atoa ratiba ya kikosi hicho, Abel afichua siri ya kambi

KUTOKA ISMAILIA: “Mwaka jana Fadlu alikuwa ni mgeni lakini mwaka huu ameshakuwa mwenyeji na ameshajua karibu wachezaji wote” Kocha msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola amesema ushindani ni mkubwa ndani ya kikosi hicho kwasababu kila mchezaji anataka kuonesha uwezo wake. Matola pia ametoa ratiba ya kikosi hicho watakapofika jijini Cairo. Mchezaji Saleh Karabaka anasema kuingia kwenye maji yenye barafu ni shughuli nzito kwake, ni lazima pawepo watu watatu kumshika. Wachezaji wengine waliozungumzia maendeleo ya kambi hiyo ni pamoja na Bajaber Mohamed, Morice Abraham pamoja na Hussein Abel ambaye amefichua namna wachezaji ‘walivyoamka’ kambini. #Simba