KUTOKA MISRI | “….hakuna kiumbe yeyote anayeweza kujiita Eliiiii zaidi ya Simba SC” Kikosi cha Simba SC kikiwa kambini nchini Misri, jioni ya leo kimepiga tizi lililomuhusisha pia kiungo wao Elie Mpanzu ambaye ameripoti kambini hapo leo… Katika tizi hizo hilo, meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyemamu amefafanua machache kuhusu utata uliokuwepo juu ya mchezaji huyo, akisema “…ni propaganda…ni Gen-z ambao wameingia kwenye mfumo wa kisasa wa mpira” Rweyemamu amesema klabu hiyo haiwezi kufanya makosa ya kumsajili mchezaji wa aina hiyo kwa mkataba wa miezi sita na kusisitiza kuwa “…Elie Mpanzu yupo, na ataendelea kuwepo hadi Simba itakavyoamua vinginevyo