#YANGAVSLIPULI GOLI la MAKAMBO YANGA VS LIPULI 1 -0 Timu ya Yanga imeendeleza moto wake ndani ya Ligi kuu baada ya kufankiwa kushinda mchezo wake wa leo dhidi ya Lipuli uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga wamecheza michezo tisa mpaka sasa wakiwa wameshinda michezo nane na kutoa sare mchezo mmoja tu dhidi ya Simba. Mchezo huo ambao Lipuli walizidiwa maarifa kipindi cha kwanza baada ya kuweza kuruhusu bao la mapema lililofungwa na Herietier Makambo dakika ya tisa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mrisho Ngassa. Ushindi huo unawarejesha nafasi ya pili ambayo ilikuwa imekaliwa na Simba, Yanga wamecheza michez 9 na kujikusanyia pointi 25 huku Simba wakiwa na Pointi 23 na vinara wa ligi Azam wamekusanya pointi 27. SUBSCRIBE: Global TV Online: https://goo.gl/nQY3hy Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars OKWI, CHAMA, KWASI NA SALAMBA WOTE WAFUNGA SIMBA SC YAIKANDAMIZA ALLIANCE FC 5-1 TAIFA MABINGWA watetezi, #SimbaSC wamepata ushindi wa kishindo baada ya kuichapa 5-1 #AllianceFC katika mchezo wa #LigiKuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikiziwa pointi nne na vinara, Azam FC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi. Watani wao wa jadi, Yanga SC wanafuatia kwa pointi zao 19 na kesho watacheza mechi yao ya nane kwa kumenyana na KMC Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa. Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi alifunga bao la kwanza dakika ya 10 kwa kichwa akimalizia pasi ya kocha baada ya krosi ya beki Mghana, Nicholas Gyan baada ya kona fupi kutoka upande wa kulia. Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan/Shomari Kapombe dk46, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Pascal Wawa, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Hassan Dilunga dk61, Clatous Chama, Adam Salamba/Meddie Kagere dk75, John Bocco na Emmanuel Okwi. Alliance FC; Kelvin Richard, Israle Patrick, Hance Masoud, Wema Sadock, Geoffrey Luseke, Juma Nyangi, Dickson Ambundo, Balama Mapinduzi/Martin Kiggi dk89, Michael Chinedu/Juhudi Philemon dk61, Jamal Mtegeta/Zabona Khamis dk80 na Siraj Juma. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA SC imeamsha makali yake baada ya kuichapa African Lyon ya Dar es Salaam mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam usiku wa leo. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, ikijivuta hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Azam FC pointi 15 za mechi saba, Singida United pointi 16 mechi tisa na Mtibwa Sugar pointi 17 mechi tisa. Ushindi wa leo wa Simba SC umetokana na mabao ya kiungo mzalendo, Shiza Ramachani Kichuya kipindi cha kwanza na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi kipindi cha pili, wakati bao la Lyon limefungwa na Awadh Juma dakika ya 62. Kichuya ambaye ameporomoka kiasi cha kuachwa timu ya taifa, leo aliamsha makali yake kwa kufunga bao la kwanza mapema tu dakika ya nane akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC leo imepata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Yanga imeanza mapema kutikisa nyavu za Stand baada ya Mrisho Ngasa kuitanguliza kwa bao la dakika ya 2, kabla ya Stand kusawazisha kupitia kwa Alex Kitenge dakika ya 15. Mchezo ulizidi kuwa mkali ambapo Yanga walipata mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Ibrahim Ajib dakika ya 32 na Andrew Vincent dakika ya 35 matokeo yaliyodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kutangulia kufunga bao la nne kupitia kwa Deus dakika ya 57 akiitumia vyema pasi aliyopewa kwa kichwa kutoka Ibrahim Ajib, lakini Stand United walijibu na kufunga bao la pili dakika ya 59 kupitia kwa Alex kitenge tena. Wakati wengi wakidhani kuwa matokeo ni 4-2, Alex Kitenge aliifungia Stand bao la tatu na kufanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu, matokeo yakiwa 4-3. Matokeo hayo yanaifanya Yanga ifikishe pointi 6 baada ya kushinda mechi zake zote mbili ikiwa nafasi ya saba huku Stand wakiwa nafasi ya tisa na pointi 6.
Timu ya Ruvu Shooting leo ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mabatini mkoani Pwani, imeambulia sare ya kufungana goli 1-1 na Mwadui FC katika mchezo pekee wa raundi ya 27 ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ambayo imeanza hii leo. Katika mchezo huo mchezaji Abdallah Seseme wa Mwadui FC ameweka rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi kwenye ligi hiyo msimu huu alipoitanguliza timu yake kwa bao la sekunde ya 12 ya mchezo. Baada ya kufungwa bao hilo, Ruvu waliongeza kasi ya mashambulizi lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa nyuma kwa bao hilo moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Ruvu kushambulia mfululizo na hatimaye kupata bao la kusawazisha dakika ya 69 kupitia kwa Fully Maganga baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa Mwadui FC. Matokeo hayo yanaifanya Ruvu Shooting kusogea hadi nafasi ya saba ikifikisha pointi 33 huku Mwadui ikibaki nafasi yake ya tisa ikiwa na pointi 30.
Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 KWA Sasa majina ya Shiza Kichuya wa Simba na Ibrahim Ajibu wa Yanga ndiyo yanayokimbiza kutokana na kazi yao wanayoifanya wakiwa uwanjani . Kwa Nyakati tofauti washambualiaji hao ambao walicheza pamoja na simba msimu uliopita wamefunga mabao matano. Kila mmoja ameisaidia timu yake mwejye mechi zake tofauti wote wameshacheza mechi tisa hadi sasa ambapo mabao hayo wameyafunga kwenye viwanja vya Dar na vile vya mkoani . Ajibu yeye amefunga mbele ya Njombe Mji (Njombe) ,Ndanda Dar Kagera Sugar na Stand United (Kagera) na Stand United Shinyanga akifunga mara mbili . Kwa Kichuya amefikisha mabao matano kwenye mechi dhidi ya Ruvu Shooting (Dar), Mbeya City (Mbeya) ,Kwenye kila Mechi amabzo wamefunga timu zao zilizoondoka na pointi tatu au moja. FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli...
Mabingwa wa ligi ya KPL, Tusker watakuwa na kibarua kigumu hapo kesho watakapo menyana na Gor Mahia katika mechi ya ligi ya premia nchini. Mechi hiyo itang'oa nanga mwendo wa saa moja katika uga wa nyayo. mechi hiyo ni muimu kwa timu hizo mbili. Tusker wako katika nafasi ya saba na alama saba kutokana na mechi nne ilhali Gor Mahia wamejipata katika nafasi ya 13 na alama tatu kutoka mechi tatu. Klabu ya AFC Leopards watakuwa wakitazama mechi hiyo kwa maakini sana kwani maasimu hao wamepangiwa kukutana siku ya jumapili katika mechi yenye msisimko. Kwa sasa, leopards wanaongoza jedwali wakiwa na alama 13 na matokeo ya mechi ya kesho haiwatishi. Tusker nao watakuwa wakicheza kwa uangalifu kwani wanakibarua siku ya jumamosi dhidi ya karuturi katika uwanja wa Nyayo. Sofapaka ambao wako katika nafasi ya pili, alama mbili nyuma ya AFC Leopards wamepangiwa kucheza Western Stima siku ya jumapili. Western Stima watatoana kijasho na Ranger Jumatano kuanzia saa tisa ugani Nyayo