Bao la Medie Kagere: Simba SC 1-0 Azam FC (VPL – 23/10/2019)
Bao la Medie Kagere: Simba SC 1-0 Azam FC (VPL – 23/10/2019)

Bao pekee la straika Mnyarwanda Medie Kagere limetosha kuipa Simba pointi tatu muhimu mbele ya matajiri wa Chamazi, Azam FC. Ni katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ukiifanya Simba kusalia kileleni ikiwa na pointi zake 15 baada ya kushinda mechi zake zote 5. Azam FC yenyewe imepoteza mchezo wake wa kwanza baada ya kushinda mechi zote tatu zilizopita na hivyo kubaki kwenye nafasi ya sita na pointi tisa katika michezo minne.



KOCHA TRIANGLE Awaacha Midomo Wazi AZAM 'HAIKUWA RAHISI'
KOCHA TRIANGLE Awaacha Midomo Wazi AZAM 'HAIKUWA RAHISI'

KOCHA TRIANGLE Awaacha Midomo Wazi AZAM 'HAIKUWA RAHISI' MCHEZO wa kwanza hatua ya Kwanza kwenye Kombe la Shirikisho kwa kikosi cha Azam FC dhidi ya Triangle United umeongezeka uzito kwa wawakilishi wa Tanzania baada ya kupoteza mchezo. Bao pekee la wapinzani wa Azam FC, Triangel United ya Zimbabwe lilifungwa dakika ya 34 na Ralph Kawondera kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi wa Azam FC. Licha ya Azam FC kupewa sapoti kubwa na mashabiki waliojitokeza uwanja wa Azam Complex hayakuzaa matunda kwani safu ya ulinzi ya Triangle United ilikuwa ngumu na ikajilinda na hatari zote. Sasa Azam FC ina kazi nzito ya kwenda kutafuta matokeo ugenini kwenye mchezo wa marudiano unaoatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 27-29 nchini Zimbabwe. Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza wa kimataifa kwa Azam FC kupoteza kwa mara ya kwanza uwanja wa nyumbani kati ya tisa ambayo walishaicheza tangu mwaka 2008. Mzigo wa Azam Fc kwa sasa ni kuongeza spidi ya kutafuta mabao zaidi ya mawili kwenye mchezo wa marudio. https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App:



Baada ya Simba Kufungwa 2-0 na JS SOURA, Hesabu Zaibeba Caf
Baada ya Simba Kufungwa 2-0 na JS SOURA, Hesabu Zaibeba Caf

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MAKOSA ya safu ya ulinzi ya Simba, jana yaliigharimu timu hiyo na kujikuta ikipigwa mabao 2-0 na JS Saoura nchini Algeria lakini wamesisitiza kwamba nguvu zote sasa ni kwa AS Vita Jumamosi. Simba sasa imeelekeza nguvu zote kwenye mechi ya AS Vita ili kucheza karata ya mwisho ya kutafuta nafasi ya kufuzu robo fainali. Hesabu zinaibeba Simba kwani ikishinda mchezo huo itafi kisha pointi tisa na kusonga mbele. Kwenye mechi ya jana safu ya ulinzi ya Simba chini ya Paschal Wawa, Mohammed Tshabalala na Paul Bukaba haikuwa na uelewano mzuri jambo ambalo liliwapa Saoura nguvu ya kushambulia. Mabao ya wenyeji yalifungwa na Yahya Sherrif kwa shuti la kiufundi huku la pili likipachikwa na Mohammed Amine kwa penalty. Amine alifanyiwa faulo na Bukaba ambaye kipindi cha kwanza nusura ajifunge alipokuwa akiokoa. Sasa Simba imeelekeza nguvu zake kwa mechi ya Jumamosi saa moja usiku kwenye Uwanja wa Taifa ambayo wamesisitiza kwamba hata kama Mwinyi Zahera wa Yanga atauza siri zao kwa Vita potelea mbali lakini ushindi lazima. Kocha wa Simba,Patrick Aussems amefunga ukurasa wa mchezo wa jana na kuanzia leo ni kazi moja tu huku mashabiki nao wakisisitiza kupambana. Zahera aliliambia Spoti Xtra kwamba; “Simba atamfunga Vita kwenye Uwanja wa Taifa na wanaweza kwenda robo fainali, lakini haiwezi kubeba ubingwa wa Afrika.” “Haina timu yenye uwezo huo. Lakini ni ukweli usiofi chika kwamba mimi Vita nitawapa mbinu za Simba kwavile wale ni rafi ki zangu na kocha wao ni bosi wangu kwenye timu ya Taifa. “Siwezi kuwafi cha, ila itakuwa ni mechi ngumu sana na nzuri,”alisema Zahera ambaye anadai kwamba Simba inamuombea mabaya kwenye Ligi Kuu na FA. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars



AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 05/03/2019)
AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 05/03/2019)

African Lyon wameendelea kupoteza matumaini ya kusalia ligi kuu Tanzania Bara baada ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania, katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba l Uhuru Dar es Salaam. Wageni JKT ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kupitia kwa Hassan Mwaterema kabla ya Hood Mayanja aliyeingia dakika ya 72, kuisawazishia Lyon dakika ya 75. Kwa matokeo hayo JKT Tanzania imepanda kutoka nafasi ya tisa hadi ya sita ikiwa na pointi 36 sawa na Mbao FC pamoja na Alliance FC huku African Lyon ikiendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22.



MAGOLI: AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA (TPL - 05/03/2019)
MAGOLI: AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA (TPL - 05/03/2019)

African Lyon wameendelea kupoteza matumaini ya kusalia ligi kuu Tanzania Bara baada ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania, katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba l Uhuru Dar es Salaam. Wageni JKT ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kupitia kwa Hassan Mwaterema kabla ya Hood Mayanja aliyeingia dakika ya 72, kuisawazishia Lyon dakika ya 75. Kwa matokeo hayo JKT Tanzania imepanda kutoka nafasi ya tisa hadi ya sita ikiwa na pointi 36 sawa na Mbao FC pamoja na Alliance FC huku African Lyon ikiendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22.



MAGOLI YOTE: MWADUI FC 1-2 YANGA SC (TPL – 22/11/2018)
MAGOLI YOTE: MWADUI FC 1-2 YANGA SC (TPL – 22/11/2018)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC leo wamepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wao wa kwanza nje ya Dar es Salaam kwenye ligi msimu huu, na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote hadi sasa. Yanga ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 10 kupitia kwa Heritier Makambo, kabla ya Mwadui kusawazisha dakika ya 40 kupitia kwa Salim Aiyee akitumia makosa ya kipa wa Yanga Klaus Kindoki, lakini mkongwe Mrisho Ngasa akaamua matokeo kwa kuifunga Yanga bao la pili dakika ya 58. Katika mchezo huu kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alilazimika kufanya mabadiliko kwa kumuweka nje kipa Klaus Kindoki na nafasi yake ikachukuliwa na Ramadhan Kabwili, Amissi Tambwe nafasi yake ikachukuliwa na Raphael Daud, na Gadiel Michael nafasi ikachukuliwa na Pato Ngonyani. Matokeo haya yanaifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili ikifikisha pointi 29 katika michezo 11 iliyocheza ambapo imetoka sare michezo miwili na kushinda michezo tisa.



Kagera vs Azam FC Post Match Press | Azam FC yajipanga kuendelea na moto TPL
Kagera vs Azam FC Post Match Press | Azam FC yajipanga kuendelea na moto TPL

BENCHI la ufundi la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, limejipanga vilivyo kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kisawasawa ili kuendelea na rekodi nzuri waliyoanza katika Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu huu. Azam FC iliyoichapa Kagera Sugar leo bao 1-0 lililofungwa na Donald Ngoma, ipo kileleni kwa takribani wiki nne sasa ikifikisha jumla ya pointi 30 baada ya ushindi wa mechi tisa na sare tatu huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja. #AzamFCUnbeaten #AzamFCPopoteInakanyaga



KOCHA Yanga Awalipua Wachezaji/ Amtaja Tambwe, Ajibu
KOCHA Yanga Awalipua Wachezaji/ Amtaja Tambwe, Ajibu

KOCHA Yanga Awalipua Wachezaji/ Amtaja Tambwe, Ajibu Timu ya Yanga imeendeleza moto wake ndani ya Ligi kuu baada ya kufankiwa kushinda mchezo wake wa leo dhidi ya Lipuli uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga wamecheza michezo tisa mpaka sasa wakiwa wameshinda michezo nane na kutoa sare mchezo mmoja tu dhidi ya Simba. Mchezo huo ambao Lipuli walizidiwa maarifa kipindi cha kwanza baada ya kuweza kuruhusu bao la mapema lililofungwa na Herietier Makambo dakika ya tisa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mrisho Ngassa. Ushindi huo unawarejesha nafasi ya pili ambayo ilikuwa imekaliwa na Simba, Yanga wamecheza michez 9 na kujikusanyia pointi 25 huku Simba wakiwa na Pointi 23 na vinara wa ligi Azam wamekusanya pointi 27. SUBSCRIBE: Global TV Online: https://goo.gl/nQY3hy Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho




« Previous Next »


Popular Tags

#Paul George  #Zlatan Ibrahimovi  #Miami Heat  #Best Football Defending Skills  #Lionel Messi  #Kevin Durant  #LeBron James  #Stephen Curry  #Best Ball Controls  #Manuel Neuer  

Popular Users

#rihanna  #incarceratedbob  #TheEllenShow  #selenagomez  #oldhossradbourn  #blakegriffin23  #ArianaGrande  #StephenCurry30  #JohnCena  #SteveNash  #floydmayweather  #JJWatt  #DjokerNole  #rolopez42  #NASA