Content removal request!


MAGOLI: AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA (TPL - 05/03/2019)

African Lyon wameendelea kupoteza matumaini ya kusalia ligi kuu Tanzania Bara baada ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania, katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba l Uhuru Dar es Salaam. Wageni JKT ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kupitia kwa Hassan Mwaterema kabla ya Hood Mayanja aliyeingia dakika ya 72, kuisawazishia Lyon dakika ya 75. Kwa matokeo hayo JKT Tanzania imepanda kutoka nafasi ya tisa hadi ya sita ikiwa na pointi 36 sawa na Mbao FC pamoja na Alliance FC huku African Lyon ikiendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22.