Clatous Chama ameifungia Simba goli la kusawazisha dakika ya 90 na kufanya matokeo yawe ni sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba, Mwanza. Katika mchezo huo mkali, Azam walitangulia kwa goli la Prince Dube dakika ya 14.
Ni mechi ya Ligi Kuu ya Vijana U20 Tanzania Bara iliyopigwa Azam Complex, Chamazi, Simba na Yanga U20 zikitoka sare ya bao 1-1. Ametangulia kufunga Juma Yusuph wa Simba dakika ya 7 kabla ya Willyson Christopher kuchomoa dakika 39. Hii ni #KariakooDerbyU20
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo wa NBC Premier League kati ya KMC FC dhidi ya Simba SC. Mchezo huo umemalizika kwa sare ya 2-2 Magoli yamefungwa na Waziri Junior kwa upande wa KMC. Saidi Ntibazonkiza na Jean Baleke wakaifungia Simba SC.
Azam FC wamecheza Mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan,katika Uwanja wa Azam Complex chamazi. Mchezo huo umemalizika kwa sare ya 1-1.