Yanga 1-1 Simba | U20 Premier League | Highlights 21/01/2024 by @Azam TV - Post Details

Yanga 1-1 Simba | U20 Premier League | Highlights 21/01/2024

Ni mechi ya Ligi Kuu ya Vijana U20 Tanzania Bara iliyopigwa Azam Complex, Chamazi, Simba na Yanga U20 zikitoka sare ya bao 1-1. Ametangulia kufunga Juma Yusuph wa Simba dakika ya 7 kabla ya Willyson Christopher kuchomoa dakika 39. Hii ni #KariakooDerbyU20

Similar Posts!

Yanga 4-1 Prisons | Magoli | NBC Premier League - 28/05/204
Yanga 4-1 Prisons | Magoli | NBC Premier League - 28/05/204

Tazama magoli yote matano yaliyofungwa kwenye mechi ya NBC Premier League kati ya Yanga SC dhidi ya Tanzania Prisons. Yanga imeshinda magoli 4-1. Stephane Aziz Ki amefunga hat trick na lingine limefungwa na Kennedy Musonda. Goli la Prisons limefungwa na Beno Ngasa



Magoli | Yanga SC 3-0 Tabora United |  NBC Premier League 25/05/2024
Magoli | Yanga SC 3-0 Tabora United | NBC Premier League 25/05/2024

Joseph Guede, Maxi Nzengeli na Stephane Aziz Ki ndiyo waliotikisa nyavu za Tabora United na kuipa Yanga ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa raundi ay 29 #NBCPremierLeague ukipigwa Benjamin Mkapa Stadium. Goli alilofunga Aziz Ki dakika ya 90 kwenye mchezo ni goli lake la 18 kwenye ligi msimu huu akizidi kukifukuzia kiatu cha ufungaji bora, akiwa na mechi moja mkononi.



Feitoto apiga mbili, Azam FC ikiifumua Kagera Sugar 5-1 Chamazi (Magoli) - NBCPL 25/05/2024
Feitoto apiga mbili, Azam FC ikiifumua Kagera Sugar 5-1 Chamazi (Magoli) - NBCPL 25/05/2024

Feisal Salum amefunga magoli mawili Azam FC ikiibugiza Kagera Sugar mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa leo kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi..... Magoli mengine kwenye mchezo huu yametoka kwa Gibril Sillah dakika ya 50’, Kipre Jr dakika ya 65' na Iddy Nado dakika ya 90, huku Feisal akifunga yake dakika ya 72 na 79.



MAGOLI: Yanga yaipiga Dodoma Jiji 4-0; Aziz Ki afikisha 17; NBC PL 22/05/2024
MAGOLI: Yanga yaipiga Dodoma Jiji 4-0; Aziz Ki afikisha 17; NBC PL 22/05/2024

Stephane Aziz Ki amefunga magoli mawili na kufikisha magoli 17 katika mbio za ufungaji bora, Yanga ikiibugiza Dodoma Jiji mabao 4-0 kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma. Ni mchezo wa #NBCPremierLeague uliofunguliwa na goli la Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Aziz kufunga mawili dakika ya 45+3 kwa penati na dakika ya 51, na kisha Maxi Nzengeli akafunga kazi kwa goli la nne dakika ya 78. Magoli yote manne haya hapa....



Magoli | Simba SC 4-1 Geita Gold | NBC Premier League 21/05/2024
Magoli | Simba SC 4-1 Geita Gold | NBC Premier League 21/05/2024

Simba SC imepata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Geita Gold FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa leo Azam Complex, Chamazi. Geita walitangulia kwa goli la Geofrey Julius dakika ya 11, kabla ya Simba kusawazisha dakika ya 45 kwa penati ya Saidi Ntibazonkiza ambaye pia alifunga la pili dakika ya 72 kwa free-kick. Aliyekamilisha mabao mawili ya mwisho ni Ladaki Chasambi dakika ya 86 na 90..... Haya hapa magoli...



Ihefu SC 0-1 Yanga SC | Highlights | Nusu Fainali CRDB Bank Federation CUP 19/05/2024
Ihefu SC 0-1 Yanga SC | Highlights | Nusu Fainali CRDB Bank Federation CUP 19/05/2024

Goli pekee la Stephane Aziz ki limeipeleka Yanga fainali yake ya tano ya michuano ya #CRDBBankFederationCup ikishinda 1-0 dhidi ya Ihefu SC, mchezo wa nusu fainali uliopigwa Sheikh Amri Abeid Arusha. Yanga sasa itakutana na Azam FC katika mchezo wa fainali, Juni 02, 2024.



Dodoma Jiji 0-1 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 17/05/2024
Dodoma Jiji 0-1 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 17/05/2024

Goli pekee la Freddy Michael Koublan limeipa Simba pointi tatu muhimu, wakiichapa Dodoma Jiji 1-0 kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma. Hii ni #NBCPremierLeague



Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC  | Highlights | NBC Premier League 13/05/2024
Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 13/05/2024

Yanga SC imeichapa Mtibwa Sugar 3-1 na kutangaza ubingwa wake wa 30 kwenye ligi kuu ya NBC Tanzania Bara ikiwa na mechi tatu mkononi baada ya kufikisha alama 71 ambazo hazifikiwi na timu nyingine. Mtibwa ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa Charles Ilanfya lakini Yanga wakachomoa dakika ya 62 kwa goli la Kennedy Musonda, Nasry Kombo akajifunga dakika ya 66 na Clement Mzize akamaliza kazi dakika ya 81. Tazama highlights...