LIVE - UCHAMBUZI KUELEKEA MECHI YA LEO BIASHARA UTD VS NDANDA SC LIGI KUU TZ BARA  (TPL - 11/3/2019)
LIVE - UCHAMBUZI KUELEKEA MECHI YA LEO BIASHARA UTD VS NDANDA SC LIGI KUU TZ BARA (TPL - 11/3/2019)

Mechi moja inapigwa leo kuanzia saa 10:00 jioni kati ya Biashara United vs Ndanda SC na itakuwa LIVE Azam Sports 2. TuKO MBASHARA kupitia #AzamSports2 , #AzamTVApp na Youtube.



Ndanda SC walivyopigwa 2-0 na Stand United: Magoli & Interviews (TPL – 06/02/2019)
Ndanda SC walivyopigwa 2-0 na Stand United: Magoli & Interviews (TPL – 06/02/2019)

Ndanda SC wamekutana na kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Stand United katika mchezo wa #LigiKuuTanzaniaBara uliopigwa jana kwenye Dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga. Mabao yote ya Stand United yamefungwa na Six Mwasekaga dakika ya 9 na 23.



KIPYENGA CHA MWISHO: "Goli moja la Simba dhidi ya JKT Tanzania halikuwa halali" (08/11/2018)
KIPYENGA CHA MWISHO: "Goli moja la Simba dhidi ya JKT Tanzania halikuwa halali" (08/11/2018)

Kwa mujibu wa kipindi hiki cha terehe 08/11/2018, bao la pili alilofunga Meddie Kagere kwenye mchezo kati ya JKT Tanzania vs Simba SC uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Jumamosi ya Novemba 2, 2018, halikuwa bao halali kwa kuwa mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga. Pamoja na matukio mengine yaliyojiri kwenye mchezo huo, pia palikuwa na matukio mawili ya wachezaji wa JKT kudai penati wakidai wachezaji wa Simba Mohamed Hussein na Erasto Nyoni kwa nyakati tofauti, walishika mpira ndani ya eneo la hatari hadi kusababisha mchezaji wa JKT Ahmed Shiboli kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Mbali na mchezo huo, kipindi hiki kimechambua mechi kdhaa za raundi ya 13 ya Ligi Kuu Tanzania Bara ukiwemo mchezo wa Yanga vs Ndanda SC na ule wa Kagera Sugar vs Azam FC. Tukio kubwa katika mchezo wa Kagera Sugar na Azam FC ni mchezaji wa Azam FC Donald Ngoma kupewa kadi nyekundu, kadi ambayo wengi hawakuelewa sababu za adhabu hiyo kumkumba. Waamuzi wawili wastaafu ambao ni magwiji, Osman Kazi na Omary Abdulkadir wamechambua matukio yote na kuonesha ni wapi waamuzi walikosea na wapi waamuzi walipatia, na nini walipaswa kufanya. Kipyenga cha Mwisho ni kila Alhamis saa 3:30 usiku Azam Sports 2.



KMC FC 1-0 MBEYA CITY ; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 05/11/2018)
KMC FC 1-0 MBEYA CITY ; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 05/11/2018)

Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja ambapo timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) leo imepata ushindi wa pili mfululizo kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Uhuru Jijini Da es Salaam. KMC leo imeinyoa Mbeya City kutoka jijini Mbeya kwa kipigo cha bao 1-0 ikiwa ni siku chache baada ya kuichapa Ndanda SC mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa Ijumaa iliyopita. Goli pekee la KMC limepatikana dakika ya 85 ya mchezo kupitia kwa Cliff Buyoya alipouwahi mpira uliopanguliwa na kipa wa Mbeya City kufuatia shuti la Emmanuel Mvuyekure. Matokeo hayo yameifanya KMC kufikisha alama 16 ikiwa nafasi ya 10.



SINGIDA UNITED 3-1 NDANDA FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 06/10/2018)
SINGIDA UNITED 3-1 NDANDA FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 06/10/2018)

Singida United ya mjini Singida imeichapa NDanda SC mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye uwanja wa Namfua Singida. Habibu Haji Kyombo ndiye aliyeing’arisha Singida kwenye mchezo huo kwa kufunga mabao mawili dakika ya 34 kwa mkaju wa penati na dakika ya 36. Ndanda walifanikiwa kupata bao moja dakika ya 75 kupitia kwa Vitalis Mayanga kabla ya Eliuter Mpepo kuifungia Singida bao la tatu kwa free-kick ya moja kwa moja dakika ya 86.



HIGHLIGHTS: NDANDA FC 0-0 SIMBA SC (TPL - 15/09/2018)
HIGHLIGHTS: NDANDA FC 0-0 SIMBA SC (TPL - 15/09/2018)

‘Wana-kuchele’ Ndanda SC leo wamevunja mwiko wa kutopata ushindi mbele ya Mnyama mkali Simba baada ya kuilazimisha suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara. Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja, wenyeji Ndanda waliingia na mbinu ya kuzuia zaidi na kuwaacha Simba wacheze mpira hasa kwenye eneo ambalo halikuwa na hatari yoyote. Mabingwa watetezi, Simba licha ya kuwaanzisha washambuliaji watatu machachari, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco, ilishindwa kutengeza nafasi za wazi kutokana na washambuliaji hao kudhibitiwa vilivyo na mabeki wa Ndanda. Hadi mwisho wa mchezo, Simba ilikuwa imepiga jumla ya mashuti 17 ambapo kati ya hayo ni mashuti matatu pekee ndiyo yaliyolenga lango, huku Ndanda wakiwa wamepiga jumla ya mashuti matatu na moja pekee likiwa ndilo limenga lango. Hii ni mara ya kwanza Ndanda FC inakataa kufungwa na Simba, tangu ipande Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2013. Baada ya mchezo huo, Nahodha wa Simba John Bocco amesema licha ya matokeo hayo kutowafurahisha, wanayasahau na kuanza kujipanga kwaajili ya mchezo ulio mbele yao huku kocha wa Ndanda Malale Hamsini akisema aliamua kutumia mbinu hiyo kutokana na ukubwa wa timu ya Simba. Matokeo hayo yanaiweka Simba katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7, huku Ndanda wakifikisha pointi 4 katika nafasi ya 12.



RATIBA! Mechi 11 Za Simba Zijazo, 5 kucheza Nyumbani
RATIBA! Mechi 11 Za Simba Zijazo, 5 kucheza Nyumbani

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Ratiba ya mechi 11 zijazo za timu ya Simba, ratiba inaonesha mechi 5 mfululizo itazipiga kwenye Uwanja wake wa nyumbani. Ndanda FC v Simba SC Mbao FC v Simba SC Mwadui FC v Simba SC Simba SC v Biashara United Simba SC v Yanga SC Simba SC v African Lyon Simba SC v Stand United Simba v Alliance FC Ruvu Shooting FC v Simba SC JKT Tanzania v Simba SC KMC FC vs Simba SC Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars




« Previous Next »


Popular Tags

#Goal Celebrations  #Football Skills  #Counter Attack Goals Football  #Mesut Ozil  #Golden State Warriors  #Shot Goals  #Paul Pogba  #Stephen Curry  #James Harden  #Cristiano Ronaldo  

Popular Users

#fauxpelini  #OleksiakPenny  #JohnCena  #iamsrk  #obj  #JLo  #BizNasty2point0  #IAmJericho  #RobbieSavage8  #LAKings  #BellaTwins  #NiallOfficial  #SportsCenter  #rolopez42  #BaileyLAKings