Azam FC imeichapa Ndanda SC jumla ya mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Azam Complex, Dar es Salaam. Wenyeji Azam ndiyo waliotawala zaidi mchezo na kufanikiwa kupa mabao hayo kupitia kwa Tafadzwa Kutinyu aliyefunga mabao mawili dakika 42 kwa mkwaju wa penati huku akifunga bao lingine dakika ya 60. Licha ya Ndanda kuamka na kuanza kusukuma mashambulizi, Joseph Mahundi aliifungia Azam bao la tatu dakika ya 79, licha ya kutokea utata wa maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi msaidizi, ambaye awali alionesha kuwa haikuwa bao.
Dakika ya 79 ya mchezo Azam wamepata bao kupitia kwa Joseph Mahundi lakini mwamuzi msaidizi akaonesha ishara kuwa halikuwa bao. Baada ya majadiliano ya sekunde kadhaa ikaamuliwa kuwa ni bao na mchezo ukaendelea. Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ukipigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam ukiwakutanisha Azam FC vs Ndanda FC.
Tafadzwa Kutinyu dakika ya 59 aliifungia Azam FC bao la pili dhidi ya Ndanda FC. Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ukipigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
Dakika ya 41 Azam FC walipata penati baada ya beki wa Ndanda kuunawa mpira ndani ya eneo la 18, na Tafadzwa Kutinyu akachukua jukumu la kupiga penati hiyo. Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ukipigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu Boniface Wambura imetangaza msimu mpya wa ligi hiyo 2018/19 kuanza kutimua vumbi rasmi tarehe 22/08/2018 ukishirikisha timu 20. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na bodi hiyo, watani wa jadi Simba na Yanga wamepangwa kukutana Septemba 30 mwaka huu ambapo Simba watakuwa wenyeji. Wambura amesema ratiba hiyo imezingatia ratiba ya michuano mingine ikiwemo michuano ya CAF itakayoanza mwezi Novemba mwaka huu, kalenda ya FIFA, Kombe la Mapinduzi pamoja na michuano ya CECAFA. Mechi ya ngao ya jamii kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi itapigwa Agosti 18, 2018 kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, na itakuwa ni kati ya mabingwa wa ligi kuu msimu uliopita Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports. Tarehe 22/08/2018: Simba SC vs Tanzania Prisons, Ruvu Shooting vs Ndanda FC, Alliance vs Mbao FC, Coastal Union vs Lipuli FC, Singida United vs Biashara, Kagera Sugar vs Mwadui FC. Tarehe 23/08/2018: Stand United vs African Lyon, JKT Tanzania vs KMC, Mtibwa Sugar vs Yanga SC, Azam FC vs Mbeya City.
Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Ndanda SC na Mwadui FC inayopigwa dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Ndanda walikuwa mbele kwa mabao 3-0. Ndanda FC ambayo inapigania kutoshuka daraja, imeanza kwa kasi na kujipatia magoli matatu ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Jacob Massawe dakika ya 3, Mrisho Ngassa dakika ya 5 na Tibar John dakika ya 40. Mabao hayo yamedumu hadi mwisho wa mchezo, na kuifanya Ndanda FC kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.