Timu ya African Lyon ambayo tayari imeshuka daraja, imejiongezea pointi moja baada ya kutoka sare na Mbeya City, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Lyon ndiyo waliotangulia kupata mabao yote mawili kupitia kwa Musht Bartoz dakika ya 21 na Awadhi Juma dakika ya 45+2 lakini Mbeya City walitumia dakika kumi za mwisho kusawazisha kupitia kwa Victor Hangaya dakika ya 82 na Mohamed Kapeta dakika ya 90+5. Matokeo hayo yameifanya Lyon kufikisha pointi 23 ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi huku Mbeya City ikifikisha pointi 47 na kupanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya saba sawa na Ndanda SC ambayo imeshuka hadi nafasi ya nane.
KOCHA Simba "TUMEJARIBU Kila Njia Tumeshindwa kwa AZAM FC Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kuwa timu yake imepambana kupata matokeo mbele ya Azam FC lakini wameshindwa huku akiwaahidi mashabiki kuchukua alama tatu katika mchezo ujao dhidi ya Mtibwa huku wakiwasubiria Ndanda kwa hamu. Kocha Aussems amesema tulijaribu kupita kushoto na kulia kutafuta goli lakini haikuwezekana. #KOCHASIMBA #SIMBAVSAZAM https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
Timu ya Mbao FC imefufua matumaini ya kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda SC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Bao pekee la ushindi la Mbao FC limefungwa na Said Hamis Said Jr dakika ya 57 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea mpira uliopigwa kutoka kwa kipa wake Bruno Thomas na kuwatoka mabeki wa Ndanda. Ushindi huo umeitoa Mbao kutoka nafasi ya 19 hadi ya 13 ikifikisha pointi 40 huku Ndanda ikisalia na pointi 43 nafasi ya saba.
Azam FC wamekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Ndanda SC kwenye mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara iliyochezwa leo jioni Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara. Bao pekee la Ndanda limefungwa na Mohamed Mkopi dakika ya 62 akimalizia kwa kichwa mpira wa ‘free-kick’ uliopigwa na Kigi Makasi nje kidogo ya eneo la 18. Ushindi huo wa Ndanda SC dhidi ya Azam FC umeibeba kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya sita ikifikisha pointi 43 huku Azam FC ikiendelea kusalia kwenye nafasi ya pili na pointi zake 66.
Azam FC wamekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Ndanda SC kwenye mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara iliyochezwa leo jioni Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara. Bao pekee la Ndanda limefungwa na Mohamed Mkopi dakika ya 62 akimalizia kwa kichwa mpira wa ‘free-kick’ uliopigwa na Kigi Makasi nje kidogo ya eneo la 18. Ushindi huo wa Ndanda SC dhidi ya Azam FC umeibeba kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya sita ikifikisha pointi 43 huku Azam FC ikiendelea kusalia kwenye nafasi ya pili na pointi zake 66.
Simba SC yaibwaga Coastal Union kwenye dimba lake la Mkwakwani na Yanga SC walizwa na Mtibwa Sugar Morogoro. Kesho ni zamu ya Azam FC dhidi ya Ndanda mkoani Tabora. Kwa hayo na mengine mengi ya kimichezo ungana na Ahmed Ally ndani ya Mshikemshike Viwanjani.
Dakika nane za kipindi cha pili zimetosha kuipa Biashara United ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma. Mabao ya wenyeji Biashara United yamefungwa na Tariq Seif dakika ya 51 na George Makang’a dakika ya 58. Ushindi huu umeiongezea pointi tatu muhimu Biashara United, na kufikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kusalia katika nafasi ya 19 juu ya African Lyon yenye pointi 22 na Ndanda SC yenye pointi 33 katika nafasi ya 17.
#Biasharaunitedfc vs #Ndandafc magoli yote yapo hapa. Usisahau Ku subscribe video nyiñgine zinakuja hivi punde.