Azam FC wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Azam Complex imeendeleza dozi ya ushindi mnono kwa kuitandika Singida United mabao 4-0. Magoli ya Azam yamefungwa na Ramadhani Singano dakika ya 66, Joseph Mahundi dakika ya 74 na Donald Ngoma aliyefunga mawili dakika ya 77 na 90. Kwa ushindi huo Azam imefikisha alama 59 ikiwa nyuma ya alama nane dhidi ya vinara Yanga.
Azam FC wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Azam Complex imeendeleza dozi ya ushindi mnono kwa kuitandika Singida United mabao 4-0. Magoli ya Azam yamefungwa na Ramadhani Singano dakika ya 66, Joseph Mahundi dakika ya 74 na Donald Ngoma aliyefunga mawili dakika ya 77 na 90. Kwa ushindi huo Azam imefikisha alama 59 ikiwa nyuma ya alama nane dhidi ya vinara Yanga.
UTANI: WAWA Alivyompiga Ngumi Mkude Kikosi cha Simba Kikirejea Msimamo unaonyesha kwamba JS Saoura inaongoza kundi ikiwa na pointi nane, ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi saba, sawa na timu inayoshika nafasi ya tatu, AS Vita ambayo nayo ina pointi saba, na Simba ghafla imeporomokea mkiani ikiwa na pointi sita. Hata hivyo, Simba ina nafasi ya kusonga mbele kama itaitumia vizuri mechi yao inayofuata ya nyumbani, itakayochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba inatakiwa ikusanye nguvu zote kwa ajili ya kuzitumia kwenye mchezo huu wa mwisho, maana sasa inahitaji ushindi tu wa aina yoyote ili kutinga robo fainali bila kuangalia matokeo mengine kati ya Al Ahly na JS Saoura, Waarabu watakaochinjana wenyewe. #SIMBASC https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
Dakika nane za kipindi cha pili zimetosha kuipa Biashara United ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma. Mabao ya wenyeji Biashara United yamefungwa na Tariq Seif dakika ya 51 na George Makang’a dakika ya 58. Ushindi huu umeiongezea pointi tatu muhimu Biashara United, na kufikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kusalia katika nafasi ya 19 juu ya African Lyon yenye pointi 22 na Ndanda SC yenye pointi 33 katika nafasi ya 17.
Hatimaye wakata miwa wa Mtibwa, timu ya Mtibwa Sugar wamepata ushindi wa kwanza baada ya takriban mechi nane za ligi kuu Tanzania Bara, wakiichapa Coastal Union mabao 3-1 kwenye uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro. Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Ayoub Lyanga dakika ya 21, lakini wenyeji Mtibwa wakasawazisha kupitia kwa Dickson Daud dakika ya 40, kabla ya Jaffary Kibaya kupachika bao la pili dakika ya 55 na Riphat Khamis dakika ya 67. Ushindi huo umeifanya Mtibwa ipande juu kwa nafasi sita kutoka nafasi ya 17 hadi ya 11 baada ya kufikisha pointi 32.
CHIRWA, Kikosi cha AZAM Kilivyowasili UWANJANI Kuwavaa SIMBA!! Timu ya Azam FC imetua kibabe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Simba ukiwa ni mchezo wao wa kwanza kukutana msimu huu katika ligi kuu. Simba inaingia katika mchezo dhidi ya Azam FC ikiwa na viporo vya mechi nane hadi sasa kwenye ligi hiyo baada ya kucheza mechi 17 na kupata pointi 42, Yanga ikiwa na michezo 25 na pointi 61, Azam ina mechi 24 na pointi 50. #SIMBAVsAZAM https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
Timu ya Mwadui FC imeendeleza wimbi lake la ushindi kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Mwadui Complex baada ya leo kuichapa Biashara United mabao 2-1 katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara. Mwadui walianza kupata bao dakika ya 45 kwa tiki taka ya Salim Salim Aiyee na kisha Biashara kusawazisha dakika ya 51 kwa penati iliyopigwa na Wazir Rashid Jr kabla ya Salim Aiyee kufunga bao la ushindi dakika ya 64 akimalizia krosi ya Ditram Nchimbi. Mwadui wamefikisha pointi 33 baada ya kuchezo mechi 28 na kukaa katika nafasi ya nane huku Biashara wakisalia katika nafasi yake ya 19 na pointi 23 katika michezo 26 waliyocheza.
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars KIKOSI cha Yanga, leo kimepoteza mchezo wake wa kombe la SportPesa ikiwa ni hatua ya robo fainali kwa kukubali kufungwa mabao 3-2 dhidi ya KK Sharks ya Kenya mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa. Michuano ya SportPesa Cup ambayo kwa sasa ni msimu wake wa tatu imeshirikisha timu nane ikiwa ni nne kutoka Tanzania ambazo ni Singida United, Simba, Mbao na Yanga na zile za kutoka Kenya ni pamoja na KK Sharks, Bandari, AFC Leopards na Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi. Kipindi cha kwanza Yanga walikubali kupoteza kutokana na uzembe wa mabeki ambapo dakika ya 9 KK Sharks waliandika bao la kwanza kupitia kwa Abuye Duke na baada ya kuzidisha mashambulizi wakaandika bao la pili dakika ya 37 kupitia kwa Abege George. Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika Yanga walikuwa nyuma kwa mabao mawili, kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko kwa kumtoa Haruna Moshi na kuingia Amiss Tambwe pamoja na Abdallah Shaibu na kuingia Thaban Kamusoko, Mrisho Ngassa nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke pamoja na Paul Godfery nafasi yake kuchukuliwa na Juma Abdul kasi ya Yanga ilianza kuonekana. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars/ Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars/ Twitter: https://twitter.com/kidanistars