Timu ya Mwadui FC imeendeleza wimbi lake la ushindi kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Mwadui Complex baada ya leo kuichapa Biashara United mabao 2-1 katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara. Mwadui walianza kupata bao dakika ya 45 kwa tiki taka ya Salim Salim Aiyee na kisha Biashara kusawazisha dakika ya 51 kwa penati iliyopigwa na Wazir Rashid Jr kabla ya Salim Aiyee kufunga bao la ushindi dakika ya 64 akimalizia krosi ya Ditram Nchimbi. Mwadui wamefikisha pointi 33 baada ya kuchezo mechi 28 na kukaa katika nafasi ya nane huku Biashara wakisalia katika nafasi yake ya 19 na pointi 23 katika michezo 26 waliyocheza.