Azam FC wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Azam Complex imeendeleza dozi ya ushindi mnono kwa kuitandika Singida United mabao 4-0. Magoli ya Azam yamefungwa na Ramadhani Singano dakika ya 66, Joseph Mahundi dakika ya 74 na Donald Ngoma aliyefunga mawili dakika ya 77 na 90. Kwa ushindi huo Azam imefikisha alama 59 ikiwa nyuma ya alama nane dhidi ya vinara Yanga.