Hatimaye wakata miwa wa Mtibwa, timu ya Mtibwa Sugar wamepata ushindi wa kwanza baada ya takriban mechi nane za ligi kuu Tanzania Bara, wakiichapa Coastal Union mabao 3-1 kwenye uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro. Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Ayoub Lyanga dakika ya 21, lakini wenyeji Mtibwa wakasawazisha kupitia kwa Dickson Daud dakika ya 40, kabla ya Jaffary Kibaya kupachika bao la pili dakika ya 55 na Riphat Khamis dakika ya 67. Ushindi huo umeifanya Mtibwa ipande juu kwa nafasi sita kutoka nafasi ya 17 hadi ya 11 baada ya kufikisha pointi 32.