Prince Dube ameifunga Simba kwa mara ya tatu msimu huu, Azam FC wakishinda mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports #AzamSportsFederationCup , mechi ikipigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Azam walianza kwa goli la Lusajo Mwaikenda dakika ya 22 na Simba kusawazisha dakika ya 28 kupitia kwa Sadio Kanoute kabla ya Dube kumaliza kazi dakika ya 75.
Kuna #hattrick kutoka kwa Jean Baleke dakika ya 28 za kwanza na pia kuna mengine mawili kutoka kwa Saidi Ntibazonkiza na Pape Ousman Sakho dakika ya 40 na 90+5… Simba wakapata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ihefu SC kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Ni mechi ya robo fainali ya #AzamSportsFederationCup ikishuhudia Ihefu wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Raphael Daud Loth dakika ya 61 na Simba kwenda nusu fainali ambako watakutana na Azam FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
SUBSCRIBE HAPO JUU tembelea WEBSITE YETU https://bmtvtanzania.com/ INSTAGRAM https://www.instagram.com/bmtvtanzania FACEBOOK https://www.facebook.com/bmtvtanzania TWITTER https://twitter.com/bmtvtanzania1