Content removal request!


Azam 2-1 Simba | Highlights | Nusu Fainali ASFC | 07/05/2023

Prince Dube ameifunga Simba kwa mara ya tatu msimu huu, Azam FC wakishinda mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports #AzamSportsFederationCup , mechi ikipigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Azam walianza kwa goli la Lusajo Mwaikenda dakika ya 22 na Simba kusawazisha dakika ya 28 kupitia kwa Sadio Kanoute kabla ya Dube kumaliza kazi dakika ya 75.