Magoli ya Mtibwa ikiibanjua Biashara United 2-0 NBC Premier League 12/12/2021
Magoli ya Mtibwa ikiibanjua Biashara United 2-0 NBC Premier League 12/12/2021

Mtibwa Sugar imepata ushindi wake wa kwanza leo kwa kuitandika Biashara United mabao 2-0 katika mchezo wa #NBCPremierLeague uliochezwa kwenye Dimba la Manungu, Turian Morogoro. Goli la kwanza kwa Mtibwa ilikuwa ni penati ya Nzigamasabo Styve huku goli la pili likiwekwa nyavuni na Said Ndemla.



Goli la Mtibwa Sugar ikiipigisha kwata JKT (1-0) - VPL 19/12/2020
Goli la Mtibwa Sugar ikiipigisha kwata JKT (1-0) - VPL 19/12/2020

Wakata miwa wa Manungu Mtibwa Sugar imeiduaza JKT Tanzania kwa kuifunga JKT Tanzania bao 1-0 kwenye mchezo wa VPL. Tufuatilie kwenye mitandao mingine ya kijamii:- ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz



MAGOLI YOTE: MTIBWA SUGAR 3-1 COASTAL UNION (TPL - 26/02/2019)
MAGOLI YOTE: MTIBWA SUGAR 3-1 COASTAL UNION (TPL - 26/02/2019)

Hatimaye wakata miwa wa Mtibwa, timu ya Mtibwa Sugar wamepata ushindi wa kwanza baada ya takriban mechi nane za ligi kuu Tanzania Bara, wakiichapa Coastal Union mabao 3-1 kwenye uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro. Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Ayoub Lyanga dakika ya 21, lakini wenyeji Mtibwa wakasawazisha kupitia kwa Dickson Daud dakika ya 40, kabla ya Jaffary Kibaya kupachika bao la pili dakika ya 55 na Riphat Khamis dakika ya 67. Ushindi huo umeifanya Mtibwa ipande juu kwa nafasi sita kutoka nafasi ya 17 hadi ya 11 baada ya kufikisha pointi 32.



MTIBWA SUGAR 1-1 AFRICAN LYON; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 08/02/2019)
MTIBWA SUGAR 1-1 AFRICAN LYON; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 08/02/2019)

Goli la dakika ya mwisho ya mchezo limeiokoa Mtibwa Sugar kwa kuipa sare ya bao 1-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa manungu Complex, mkoani Morogoro. Bao hilo la kusawazisha limefungwa na Jaffary Salum Kibaya akimalizia kwa kichwa kona iliyochongwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ baada ya wageni katika mchezo huo African Lyon kutangulia kupata bao dakika ya 62 kupitia kwa mkongwe Ramadhan Chombo Redondo. Matokeo hayo yameipandisha Mtibwa kutoka nafasi ya 13 hadi nafasi ya 10 ikifikisha pointi 30 katika michezo 21 huku African Lyon ikiendelea kusalia mkiani na licha ya kufikisha pointi 20 baada ya kucheza michezo 25.



MSHIKEMSHIKE VIWANJANI      -         AZAM     TV      27/11/2018
MSHIKEMSHIKE VIWANJANI - AZAM TV 27/11/2018

Mtibwa Sugar yawalambisha sukari ya Manungu, Northern Dynamo na kuibuka na ushindi mnono nyumbani, Simba SC zamu yao kesho. Ni kweli uzalendo umeishia leo? Kwa undani wa haya na mengine lukuki ya kimichezo ungana na Fatma Chikawe ndani ya Mshikemshike Viwanjani.



Mtibwa Sugar 2-1 Mbeya City: Walichozungumza makocha na wachezaji (TPL 01/09/2018)
Mtibwa Sugar 2-1 Mbeya City: Walichozungumza makocha na wachezaji (TPL 01/09/2018)

Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imeendeleza ushindi katika dimba lake la nyumbani la Manungu baada ya leo kuifunga Mbeya City mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Mara baada ya mchezo huo, Azam TV imezungumza na makocha wa timu zote mbili Ramadhan Swanzurimo wa Mbeya City na Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar, wote wameeleza sababu za kitaalamu za matokeo hayo. Pia Azam TV imezungumza na baadhi ya wachezaji waliong’ara kwenye mchezo huo, Stamili Mbonde ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza la Mtibwa, Ismail Aidan Mhesa ambaye ni mfungaji wa bao la pili la Mtibwa na Eric Kyaruzi ambaye ni mfungaji wa bao pekee la Mbeya City.



Haya hapa magoli yote Mtibwa Sugar ikiichapa Mbeya City 2-1 Manungu (TPL 01/09/2018)
Haya hapa magoli yote Mtibwa Sugar ikiichapa Mbeya City 2-1 Manungu (TPL 01/09/2018)

Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imeendeleza ushindi katika dimba lake la nyumbani la Manungu baada ya leo kuifunga Mbeya City mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Katika mchezo huo ambao timu zote zimeonesha uwezo unaokaribiana, Mtbwa ndiyo waliotangulia kupata mabao kupitia kwa Stamili Mbonde dakika ya 9 na Ismail Mhesa dakika ya 42 huku Mbeya City walioonesha uhai zaidi kipindi cha pili wakipata bao lao dakika y 48 ya mchezo kupitia kwa Eric Kyaruzi. Haya hapa mabao yote yaliyofungwa kwenye mchezo huo.



MTIBWA SUGAR 1-2 LIPULI FC:  HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (VPL - 16/05/2018)
MTIBWA SUGAR 1-2 LIPULI FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (VPL - 16/05/2018)

Timu ya Mtibwa Sugar imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Lipuli FC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye dimba la Manungu, Morogoro. Mabao yote ya Lipuli yamefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 17 na 71, huku la Mtibwa likifungwa na Riffat Khamis dakika ya 53..




« Previous Next »


Popular Tags

#Cristiano Ronaldo  #Manuel Neuer  #Best Ball Controls  #Best Football Defending Skills  #Kevin Durant  #Shot Goals  #Paul George  #Franck Ribery  #Zlatan Ibrahimovi  #Best Football Defending Skills  

Popular Users

#BrunoMars  #RobbieSavage8  #Harry_Styles  #TheEllenShow  #si_vault  #katzm  #KingJames  #geniebouchard  #ATLHawks  #nfl  #ddlovato  #espn  #_BAnderson30_  #JLo  #incarceratedbob