Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imeendeleza ushindi katika dimba lake la nyumbani la Manungu baada ya leo kuifunga Mbeya City mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). Katika mchezo huo ambao timu zote zimeonesha uwezo unaokaribiana, Mtbwa ndiyo waliotangulia kupata mabao kupitia kwa Stamili Mbonde dakika ya 9 na Ismail Mhesa dakika ya 42 huku Mbeya City walioonesha uhai zaidi kipindi cha pili wakipata bao lao dakika y 48 ya mchezo kupitia kwa Eric Kyaruzi. Haya hapa mabao yote yaliyofungwa kwenye mchezo huo.