Yanga SC wamebeba Kombe la Shirikisho la Azam Sports #ASFC kwa kuitandika Coastal Union penati 4-1 kufuatia sare ya mabao 3-3 katika dakika 120. Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Feisal Salum dakika ya 57, Heritier Makambo dakika 82 na Denis Nkane dakika ya 113 huku magoli yote ya Coastal Union yakifungwa na Abdul Suleiman Sopu ambaye amefunga #Hattrick dakika ya 11, 88 na 98. Katika mikwaju ya penati, Yanga wamefunga penati zote nne walizopiga kupitia kwa Yanick Bangala, Heritier Makambo, Dickson Job na Khalid Aucho huku Coastal wakipoteza penati mbili na kufunga moja kupitia kwa Victor Akpan. Fainali hii imepigwa kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha...... Kutazama full highlights... ingia hapa https://www.youtube.com/watch?v=lfnurATeApA
Idris Ilunga Mbombo amefunga #hattrick ya tatu kwenye ligi msimu huu, akiipa Azam FC ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Biashara ...
Idris Ilunga Mbombo amefunga #hattrick ya tatu kwenye ligi msimu huu, akiipa Azam FC ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Biashara ...
Simba SC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa ...
Simba SC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa ...
Makombora mawili kutoka wa Feisal Salum #Feitoto na Chiko Ushindi yaipa Yanga ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi ...
Makombora mawili kutoka wa Feisal Salum #Feitoto na Chiko Ushindi yaipa Yanga ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi ...
SAMAKIBA 2022: Team Kiba iliyo chini ya msanii Alikiba imebeba Kombe la Nifuate 2022 kwa kuichapa Team Samatta iliyo chini ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya mabao 3-3. Katika muda wa kawaida, magoli ya Team Kiba yamefungwa na Saimon Msuva aliyefunga mawili pamoja na Alikiba mwenyewe kwa penati huku magoli ya Team Samatta ayakifungwa na Kelvin John, Mbwana Samatta na Idd Gamba kwa penati. Mechi hii ni tamasha maalum la hisani kwa ajili ya kurejesha jamii ambalo hufanyika kila mwaka chini ya taasisi ya Samakiba Foundation, na mwaka huu limefanyika kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, na kushuhudia Team Kiba wakibeba ndoo.