Content removal request!


Team Samatta 3-3 Team Kiba (Pen 2-4) | Magoli, Penati & Kombe | Nifuate 18/06/2022

SAMAKIBA 2022: Team Kiba iliyo chini ya msanii Alikiba imebeba Kombe la Nifuate 2022 kwa kuichapa Team Samatta iliyo chini ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya mabao 3-3. Katika muda wa kawaida, magoli ya Team Kiba yamefungwa na Saimon Msuva aliyefunga mawili pamoja na Alikiba mwenyewe kwa penati huku magoli ya Team Samatta ayakifungwa na Kelvin John, Mbwana Samatta na Idd Gamba kwa penati. Mechi hii ni tamasha maalum la hisani kwa ajili ya kurejesha jamii ambalo hufanyika kila mwaka chini ya taasisi ya Samakiba Foundation, na mwaka huu limefanyika kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, na kushuhudia Team Kiba wakibeba ndoo.