Magoli na penati | Yanga 3-3 Coastal Union (Pen: 4-1) | Fainali ASFC 02/07/2022 by @Azam TV - Post Details

Magoli na penati | Yanga 3-3 Coastal Union (Pen: 4-1) | Fainali ASFC 02/07/2022

Yanga SC wamebeba Kombe la Shirikisho la Azam Sports #ASFC kwa kuitandika Coastal Union penati 4-1 kufuatia sare ya mabao 3-3 katika dakika 120. Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Feisal Salum dakika ya 57, Heritier Makambo dakika 82 na Denis Nkane dakika ya 113 huku magoli yote ya Coastal Union yakifungwa na Abdul Suleiman Sopu ambaye amefunga #Hattrick dakika ya 11, 88 na 98. Katika mikwaju ya penati, Yanga wamefunga penati zote nne walizopiga kupitia kwa Yanick Bangala, Heritier Makambo, Dickson Job na Khalid Aucho huku Coastal wakipoteza penati mbili na kufunga moja kupitia kwa Victor Akpan. Fainali hii imepigwa kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha...... Kutazama full highlights... ingia hapa https://www.youtube.com/watch?v=lfnurATeApA

Similar Posts!

Ihefu SC 0-1 Yanga SC | Highlights | Nusu Fainali CRDB Bank Federation CUP 19/05/2024
Ihefu SC 0-1 Yanga SC | Highlights | Nusu Fainali CRDB Bank Federation CUP 19/05/2024

Goli pekee la Stephane Aziz ki limeipeleka Yanga fainali yake ya tano ya michuano ya #CRDBBankFederationCup ikishinda 1-0 dhidi ya Ihefu SC, mchezo wa nusu fainali uliopigwa Sheikh Amri Abeid Arusha. Yanga sasa itakutana na Azam FC katika mchezo wa fainali, Juni 02, 2024.

Dodoma Jiji 0-1 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 17/05/2024
Dodoma Jiji 0-1 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 17/05/2024

Goli pekee la Freddy Michael Koublan limeipa Simba pointi tatu muhimu, wakiichapa Dodoma Jiji 1-0 kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma. Hii ni #NBCPremierLeague

Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC  | Highlights | NBC Premier League 13/05/2024
Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 13/05/2024

Yanga SC imeichapa Mtibwa Sugar 3-1 na kutangaza ubingwa wake wa 30 kwenye ligi kuu ya NBC Tanzania Bara ikiwa na mechi tatu mkononi baada ya kufikisha alama 71 ambazo hazifikiwi na timu nyingine. Mtibwa ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa Charles Ilanfya lakini Yanga wakachomoa dakika ya 62 kwa goli la Kennedy Musonda, Nasry Kombo akajifunga dakika ya 66 na Clement Mzize akamaliza kazi dakika ya 81. Tazama highlights...

Magoli | Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC | NBC Premier League 13/05/2024
Magoli | Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC | NBC Premier League 13/05/2024

Yanga SC imeichapa Mtibwa Sugar 3-1 na kutangaza ubingwa wake wa 30 kwenye ligi kuu ya NBC Tanzania Bara ikiwa na mechi tatu mkononi baada ya kufikisha alama 71 ambazo hazifikiwi na timu nyingine. Mtibwa ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa Charles Ilanfya lakini Yanga wakachomoa dakika ya 62 kwa goli la Kennedy Musonda, Nasry Kombo akajifunga dakika ya 66 na Clement Mzize akamaliza kazi dakika ya 81. Haya hapa magoli yote...

Azam FC 0-3 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 09/05/2024
Azam FC 0-3 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 09/05/2024

MZIZIMA DERBY: Simba FC imeshinda 3-0 dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC ukipigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam. Magoli yote yamefungwa kipindi cha pili akianza Sadio Kanoute dakika ya 63, Fabrice Ngoma dakika ya 77 na David Kameta dakika ya 89. Azam FC walipata penati mapema lakini walikosa kupitia kwa Feisal Salum.... lakini pia kuna utata kuhusu tukio la Azam kupata goli iliyoamuliwa kuwa ilikuwa ni off-side.

Azam FC 0-3 Simba SC | Magoli, Penati, Off-side | NBC Premier League 09/05/2024

Simba SC 2-0 Tabora United | Highlights | NBC Premier League 06/05/2024
Simba SC 2-0 Tabora United | Highlights | NBC Premier League 06/05/2024

Simba SC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Magoli ya Simba yametoka kwa Sadio Kanoute dakika ya 19 na Edwin Balua dakika ya 77.

Mashujaa FC 0 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 05/05/2024
Mashujaa FC 0 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 05/05/2024

Goli pekee kutoka kwa Joseph Guede limeipa yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC ugenini kwenye Dimba la Lake Tanganyika Kigoma, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Tazama highlights....